KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA IRINGA , SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA MAJENGO YASIYO RAFIKI NA WALEMAVU

      

 Waziri  Lukuvi  akimkabidhi  mwanafunzi  wa shule ya Msingi Kipera
Rahel Mwikonzi cheti  cha ushiriki mzuri wa siku ya  walemavu
mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa
Kamishina  wa ustawi  wa jamii Bw Dunford Makala akitoa salam zake
Viongozi  mbali mbali  wakiwa pamoja na kamati ya ulinzi  mkoa
Mwenyekiti wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu akiwa na viongozi wa chama cha  walemavu Tanzania kushoto ni makamu mwenyekiti Bi Amina Mollel na katikati ni mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa
Waziri  Lukuvi  akihutubia
Ndumbalo  akipokea  cheti  toka kwa  waziri Lukuvi 
Waziri  Lukuvi akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza  (kulia)
Waziri  Lukuvi akimakabidhi cheti  mwanafunzi mlemavu wa shule ya sekondari ya  wasichana Iringa
Katibu wa chama  cha Viziwi Tanzania Bw Shaibu  Juma akiwa katika ulingo wa  wasanii wa ngoma kutoka kikundi cha Viziwi
Walemavu  nchini  wakiwa katika maandamano  leo  wakati wa kilele  cha
siku ya  walemavu duniani kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika
mkoa  wa Iringa,kushoto ni mkalimani  wa  kujitolea  ambae ni Mtangazaji
wa radio  Nuru Fm Bw  Clement akisaidia  kuwaelekeza  walemavu hao
 
Hiki  ndicho  cheti  ambacho kampuni ya Asas  imepewa kutokana na ushiriki mzuri wa uchangiaji katika maadhimisho hayo
Waandamanaji  wakiwa katika maandamano  hayo  leo
 
Waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri  mkuu (sera na uratibu wa bunge) Wiliam Lukuvi akihutubia katika kilele  cha siku ya  walemavu duniani ,maadhimisho  yaliyofanyika katika viwanja vya kichangani mjini Iringa Kitaifa  na Lukuvi kumwakilisha  waziri mkuu Mizengo Pinda
Walemavu  wakiwa katika maadhimisho hayo kitaifa  mjini Iringa
 
Mwenyekiti wa mkoa  CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu  na mwenyekiti wa UWT  wilaya ya  Iringa mjini wakipongezwa na  waziri  Lukuvi kwa  kuunga mkono maadhimisho ya  siku ya  walemavu nchini
Makamu  mwenyekiti  wa Shivyawata Bi Amina  Mollel akipongezwa na waziri Lukuvi kwa maandalizi mazuri
Walemavu  wakiwa katika maandamano  yao leo
Askari  wa  usalama barabara  Iringa aliyefahamika kwa jina la Sarehe
Mollel akiongoza  maandamano ya  watu  wenye  ulemavu  leo   wakati  wa
maadhimisho ya siku ya  walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika
viwanja vya  kichangani  mjini Iringa na  kuhudhuriwa na waziri wa nchi
ofisi ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge Bw  Wiliam Lukuvi kwa
niaba ya  waziri mkuu Mizengo Pinda

Waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu  sera  na uratibu wa bunge Bw
Wiliam Lukuvi akimkabidhi cheti cha ushiriki Tumain  Mdegella kwa  niaba
ya ofisi za Neema Crafti mjini Iringa  wakati wa kilele  cha
maadhimisho ya  siku ya  walemavu duniani iliyofanyika kitaifa  mjini
Iringa

 Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI
imeziagiza  mamlaka  za  usafiri  wa majini na nchi kavu (SUMATRA )
nchini  kuanza mchakato  wa  kukaa na  wamiliki wa  vyombo  hivyo  ili
kuanza  uangizaji  wa vyombo  vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni
rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku  majengo ya   serikali
kujengwa bila kuwepo kwa  mchoro  unaoonyesha mazingira yanayozingatia
makundi  yote ya jamii  likiwemo la walemavu wa viungo .
 
Agizo
hilo  limetolewa na  waziri  mkuu Mizengo  Pinda wakati  wa maadhimisho
ya  siku ya  walemavu  duniani yaliyofanyika   kitaifa  katika
viwanja  vya kichangani mkoani  Iringa jana.
 
Akiwahutubia
walemavu hao na  wananchi  waliofika katika  viwanja   hivyo waziri
mkuu ,aliyewakilishwa na waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu (sera na
uratibu wa bunge)  ,Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa  jimbo la Isimani
mkoani Iringa alisema  kuwa  kimekuwepo kilio  cha muda  mwingi  kutoka
kwa  walemavu  juu ya kusaulika katika ujenzi  wa  majengo mbali mbali
ambayo yamekuwa  yakijengwa  bila kuzingatia  kundi la  watu  wenye
ulemavu jambo ambalo ni sawa na  kuwabagua watu  hao.
 
Hivyo
alisema  katika  kuona kilio  hicho  cha  walemavu  kinafanyiwa  kazi
kuanzia  sasa majengo  yote ya  serikali  zikiwemo  shule na taasisi
nyingine  kabla ya  kuanza  ujenzi  wake lazima  wasimamizi wa  ujenzi
huo kujiridhisha kwa  mchoro ambao  utaonyesha  mazingira
yatakayomuwezesha  mlemavu   kutumia jingo  hilo bila usumbufu  tofauti
na  ilivyo sasa ambapo  idadi kubwa ya majengo mazingira  yake  si
lafiki kwa  walemavu.
 
 

Ni  siku  nyingi  watu  wenye ulemavu  wamekuwa  wakilalamika juu ya
mazingira  yasiyo rafiki    katika majengo  mbali mbali …..sasa  leo
naomba  kuagiza  kuwa michoro yote inayochorwa katika majengo ya  huduma
za  kijamii  ni marufuku  kupitishwa ama  wasimamizi  wa  ujenzi
husika  kuruhusu ujenzi  iwapo mchoro hauonyeshi  kama utayajali
makundi  yote wakiwemo  walemavu…..wasimamizi  wote msikubali
kusimamia  wala  kutangaza  tenda  ya ujenzi kama ramani  yake  si
rafiki kwa  walemavu…..lakini  pia  hata  kwenye mabasi hivi
unamtegemea mtu mwenye ulemavu wa miguu ataingia vipi na baiskeli  yake
katika gari iwapo hakuna mazingira  yanayomwezesha  kuingia …. hivi
sasa  teknlojia  imezidi kukua na baadhi ya nchi  wameanza muda mrefu
kuwajali walemavu kwa kuwa na mabasi ambayo mlemavu anaingia na
baiskeli  yake  na  kushuka nayo   bila usumbufu ni vema hata Sumatra
kuangalia uwezekano wa  kuwajali  walemavu hao . pia ni vizuri  hata
nyumba  za  ibada  nazo ningeshauri baba askofu   kuangalia kuweka
mazingira ” alisema  Lukuvi.
 
Kuhusu
ombi la walemavu hao   hasa  wale  wasio sikia kuomba  serikali  kuwa
na wakalimani katika kituo cha Televisheni ya  Taifa (TBC) na vituo
vingine  vya  luninga  ili  kuwawezesha  walemavu hao nao  kuweza
kufuatilia hotuba  ya Rais mwisho  wa mwezi na mambo mengine badala ya
kutengwa ,alisema  kuwa  suala  hilo  ni  wajibu wa  serikali  kuwajali
watu  wake  hivyo tayari  imeuagiza  uongozi  wa TBC na mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA)  kulitafutia  ufumbuzi  suala  hilo la
mkalimani  hasa katika TBC .
 
Katika
hatua nyingine  Lukuvi  aliwataka  walemavu hao  ili  ombi lao la
kutazamwa katika  nafasi za  uongozi  liweze  kuzingatiwa ni  vema  wao
wenyewe  kujitokeza kwa  wingi  kuipigia  kura  katiba  iliyopendekezwa
pindi  itakapokuja kwa  wananchi kwa madai kuwa  katika  katiba   hiyo
imezingatia mambo  mengi ya kijamii likiwemo la  kuwajali  watu  wenye
ulemavu kwa  kuwatengea nafasi nyingi  zaidi  na  iwapo  katiba  hiyo
itapitishwa kazi ya msuguano wa  rushwa unaweza  kuhamia kwa  walemavu
kwa kila mmoja kutaka  kupewa nafasi.
 

Hadi  hivi  sasa ni chama cha mapinduzi (CCM) pekee ambacho  kina
wabunge wa viti maalum wa  kuteuliwa  kutoka kundi la  walemavu huku
vyama  vingine  vyote  havijawakumbuka kabisa  watu  wenye ulemavu
ukiacha  mbunge wa  jimbo la Lindi mjini pekee ambae hakupendelewa
katika ubunge  wake bali alishindwa kihalali kwa  kuchaguliwa na
wananchi  wake..nafikiri  tushirikiane  kuhakikisha katiba  hii
iliyopendekezwa  inapita  ili  tuungane pamoja katika  kujenga nchi
yetu “
 
 Katika
salam  za  walemavu waziri  wa Afya  na ustawi  wa jamii  Dkt Seil S.
Rashid  zilizotolewa kwa  niaba  yake  na mwenyekiti  wa baraza la
watu  wenye ulemavu nchini na Dunford Makala   alisema
kuwa  wizara  inaendelea   kuimarisha  ushirikiano na vyama  vya  watu
wenye ulemavu  na  shirikiasho  la vyama  vya  watu  wenye ulemavu
Tanzania (SHIVYAWATA) katika  kuhakikisha utekelezaji  wa uwekaji  wa
fursa  na haki  sawa  kwa  watu  wenye ulemavu nchini .
 
Alisema
katika  kuhakikisha ushirikiano unakuwepo  wizara yake  imezindua
baraza  la  ushauri  la Taifa  la  watu  wenye  ulemavu  toka mnamo 1
Novemba 2014 na katika  hilo  kamwe  hawataacha  kumpongeza  Rais Dkt
Jakaya Kikwete  kwa   kumteua  mwenyekiti  wa baraza hilo
 
Aidha
alisema  kuwa ni ukweli  usiopingika kuwa nchi  hii chini ya Rais Dkt
Kikwete  imefanya mambo  mengi  zaidi ya  kuwajali  watu  wenye
ulemavu  katika Nyanja  za  kiuchumi ,kiutamaduni na  kisiasa ambavyo
vyote  hivyo  kumwezesha  mlemavu kujikwamua  kimaisha
 
Hata
hivyo  alisema  ushahidi  wa yote hayo ni pamoja na kuridhia mikataba
ya kimataifa  juu ya haki  za watu wenye ulemavu , kutungwa kwa sharia
Na.9 ya mwaka 2010 ya watu  wenye ulemavu  na kanuni zake
,kuwashirikisha  watu wenye ulemavu  katika tume ya mabadiliko ya
katiba  ya Jamhuri ya  muungano wa Tanzania pamoja na kuteuliwa kwa
wajumbe 20  wenye ulemavu  katika  bunge maalumu la mabadiliko ya katiba
la mwaka 2014.
 
 
Awali
walemavu hao  katika  risala yao  iliyosomwa na makamu  mwenyekiti  wa
SHIVYAWATA  Amina Mollel  pamoja na  kuishukuru  serikali kwa jinsi
kwa  kuendelea  kuwa karibu  zaidi na  watu  wenye ulemavu kwa kushiriki
shughuli mbali mbali za  walemavu ,bado waliweza  kuishukuru  serikali
kwa kuandaa sera ya maendeleo ya  watu wenye ulemavu ya mwaka 2004,
kutambuliwa  kwa  watu wenye ulemavu katika MKUKUTA,kuwezesha kuongezeka
kwa idadi ya watu wenye ulemavu  wanaopata  elimu kuanzia shule za
msingi hadi elimu ya juu na mambo  mengine  mengi ambayo  wao kama
walemavu wamekuwa  wakiona  serikali  yao  ipo pamoja nao.
 
Sanjari
na mema  hayo bado  waliiomba serikali kuzingatia kuwapatia  walemavu
mambo muhimu katika maisha ya kila  siku ikiwa ni pamoja na kuwa na
vyombo  vya usafiri rafiki kama magari  moshi.vyombo  vya usafiri majini
,angani ,miundo mbinu katika  majengo  na viwanja  vya  ndege ambavyo
vitamwezesha mlemavu pia kuwa  huru .
 
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa maadhimisho hayo
yaliyofanyika  chini ya kauli  mbiu  isemayo ” Maendeleo endelevu
;Ahadi  ya Teknolojia  huku mkoa  wa  Iringa  ukiendelea  kuwa  bega
kwa  bega  na  walemavu ikiwa ni pamoja na  kufanya kazi karibu na
vyama  hivyo  vya  watu  wenye  ulemavu   na kuwa mkoa huo  kwa  sasa
una jumla ya  walemavu  zaidi ya 179 ,000 na  wote  serikali
imeendelea  kuwalinda na  kuwa nao pamoja.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI