KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA TATHMINI YA MWENENDO WA BUNGE LA TANZANIA KATIKA KUSHUGHULIKIA SAKATA LA FEDHA KWENYE AKAUNTI YA TEGETA ESCROW

                

 Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho ya Sera wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Halord Sungusia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tathmini ya mwenendo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow. Kushoto ni Ofisa Mipango Dawati la Uangalizi wa Serikali wa LHRC, Hussein Sengu na Wakili, Hamisi Mkindi. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
 Wakili, Hamisi Mkindi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema Mahakama isitumiwe kama kinga ya kufanya uhalifu.
 
Hayo yamebainishwa Dar es saalam leo na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho ya Sera  wa LHRC, Halord Sungusia wakati akizungumza na wanahabari alipokuwa akitoa tathmini ya mwenendo wa Bunge la Tanzania katika kushughulikia sakata la fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
 
“Mahakama ni taasisi kuu kitaifa ya kutoa haki kwa wananchi wote lakini isitumiwe na mtu au taasisi yoyote kama kinga yake ya kufanya uhalifu” alisema Sungusia.
 
Aidha alibainisha kuwa katiba ya sasa inatoa mianya mingi ya kutozingatiwa kwa miiko ya uongozi hasa baada ya kufutwa kwa azimio la Arusha na rasimu ya pili ya katiba iliweka msingi huu wa maadili ya uongozi kwa upana na kwa msisitizo.
 
Sungusia aliongeza kuwa nchi haitokuwa salama kama katiba inayopendekezwa itapitishwa kama ilivyo kuwa  kwani inayopendekezwa haizungumzii kwa mapana maadili na miiko ya viongozi wa umma, haiweki misingi bora ya uwajibikaji na kusimamia dhamana ya uongozi na kanuni za uongozi wa umma.
 
Katika hatua nyingine LHRC kimetaka wale wote ambao watabainika katika sakata la utoaji wa fedha katika akaunti hiyo wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA