MAADHIMISHO YA WIKI YA USAFIRI WA ANGA DUNIANI YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shabaani  Mwinjaka wa pili kutoka (kulia)akipata maelezo kutoka kwa Muongoza ndege kiwanja cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNIA) Mossy Kitangita wakati alipotembelea  banda la Mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA) . Maonyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani  maadhimisho hayo yanafanyika kwa siku tatu makao makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa TCAA, DK. Nyamajeje  Weggoro Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Charles Chacha.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye maonyesho ya wiki ya usafiri wa anga Duniani   wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa TCAA, maadhimisho hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka Sabini ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye maonyesho ya wiki ya usafiri wa anga Duniani   wakipata maelezo wakati wa  maadhimisho hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka Sabini ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.

 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Moses Malaki (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shabaani  Mwinjaka wa pili kutoka (kushoto ) juu ya huduma  wanazotoa   maadhimisho hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka 70 ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago. Kutoka  Kushoto ni Kaimu mwenyekiti wa bodi wa TCAA, DK. Nyamajeje  Weggoro , Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Charles Chacha,Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mtesigwa Maugo.
Mhandishi wa ndege  wakala wa ndege za serikali Trophese Mbwambo akimuelezea huduma zinazotolewa na wakala ndege za serikali Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Dk. . Shabaani  Mwinjaka wakati wa maadhimisho ya wiki ya usafiri wa anga dunuani yanayofanyika kwenye  viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka 70 ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Dk. . Shabaani  Mwinjaka (katikati) na  Kaimu mwenyekiti wa bodi wa TCAA, DK. Nyamajeje Weggoro  wakisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja Huduma za hali ya hewa ya Usafiri wa Anga (TMA) John Mayunga wakati walipotembelea banda lake kwenye maadhimisho ya wiki ya Usafiri wa Anga Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka 70 ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.
Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya usafiri wa anga, (International Civil Aviation Day) ambayo huadhimishwa Desemba 7 kila mwaka. Lengo la maadhimisho hayo ni kukuza uewelewa wa wananchi kuhusu sekta ya usafiri wa anga na namna inavyochangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mataifa mbalimbali.

Mwaka huu siku hiyo inaadhimishwa ikiwa ni miaka sabini (70) tangu kupitishwa na kusainiwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga (maarufu kama Chicago Convention) na tangu kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).  

Kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni “Miongo Saba ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Usafiri wa Anga na Kusherehekea Miaka Sabini ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago”.

Kwa Kiingreza: “Celebrating Seven Decades of Cooperative of Air Transport Progress and Celebrating 70 years of Chicago Convections.”

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kushirikiana na wadau wa sekta wameandaa shughuli mbali mbali kuadhimisha miaka sabini ya usafiri wa anga duniani.  Kwa vile tarehe 7 Desemba ni siku ya Jumapili, maadhimisho yetu yatafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Desemba.

Moja ya Shughuli zitakazofanyika katika kipindi cha maadhimisho ni maonyesho ya wadau wa usafiri wa anga kwa siku tatu, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Desemba katika viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Banana- Ukonga.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba, anatarajiwa kuwa mgeni ramsi katika  maonyesho hayo yanayolenga kutangaza shughuli za wadau wa sekta ya usafiri wa anga. Wadau hao ni pamoja na vyuo vya usafiri wa anga, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, makampuni ya ndege, Mdhibiti wa sekta na wadau wengine wanaotoa huduma kwenye viwanja vya ndege wakiwemo Swissport na Equity Aviation.

Tarehe 4 Desemba kutakuwa na kongamano la wadau wa sekta, litakaloongozwa na kauli mbiu “Miaka 70 ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga- Mikakati ya Tanzania Katika Kuimarisha Maendeleo ya Usafiri wa Anga”. Pamoja na mambo mengine kongamano litaangalia mbinu za kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini, mchango wake katika kukuza uchumi, kinga ya abiria dhidi ya majanga, mchango ya huduma ya hali ya hewa kwenye usafiri wa anga pamoja na changamoto  zinazokabili sekta hii. Kongamano litafanyikia ukumbi wa mikutano, Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga na kufunguliwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dr. JUma Malik Akil.

Katika maadhimisho haya, pia kutakuwa na safari maalum ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa kundi la watoto 20 wakiwemo wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo na wale wa kundi la mazingira maalum. Safari imelenga kuchochea udadisi wa watoto kwenye sekta ya usafiri wa anga na kuwaamasisha ili wasome zaidi na hatimae kuja kutumikia sekta ya usafiri wa anga.

Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dr. Harrison Mwakyembe, ambaye atakuwa Mgeni Rasmi siku ya kilele cha maadhimisho, tarehe 5 Desemba, atatembelea na kukagua maendeleo ya baadhi ya miradi katika sekta ya usafiri wa anga. Miradi atakayoikagua ni pamoja na Mradi wa Swissport unaohusisha ujenzi wa Bohari Maalumu la mizigo inayosafirishwa na usafiri wa anga ambayo ina uwezo wa kutunza wanyama hai. Tanzania kwa mara ya kwanza itakua na huduma za kuhifadhi wanyama hai wanaosubiri kusafirishwa au kupokelewa kupitia usafiri wa anga. Mh Waziri pia atapata nafasi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jumba la Abiria (Terminal 3) katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere. Aidha, Mh. Waziri atazindua Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania- TCAA, yaani Aviation House.

Kamati ya wadau ya maandalizi inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria kwenye maonyesho na kutumia fursa hiyo kujifunza zaidi kuhusu sekta ya  usafiri wa anga na mchango wake katika maendeleo ya huduma na uchumi wa nchi yetu. Makampuni ya ndege yanatarajiwa pia kuchukua nafasi hiyo kutoa huduma zao za tiketi wakati wa maonyesho. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI