MAKOMANDO WAWAOKOA MATEKA SYDNEY, WAMUUA MTEKAJI

Huyu ndiye mtekaji raia wa Iran, Haron Monis.
WATU watatu wameuawa akiwemo mtekaji raia wa Iran, Haron Monis aliyekuwa ameteka watu kwa zaidi ya saa 16 katika mgahawa mmoja jijini Sydney nchini Australia jana baada ya Makomando kuvamia eneo hilo. Watu wanne akiwemo polisi wamejeruhiwa wakati wa zoezi la uokoaji.
Mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza.
Mtekaji huyo alikuwa ameachiwa kwa dhamana kwa makosa mbalimbali aliyokuwa ameshitakiwa nayo. Moja ya makosa yake ilikuwa kuwatumia barua ya matusi wazazi wa wanajeshi wa Australia waliofariki wakiwa wanalitumikia jeshi la taifa hilo nchini Iraq.
Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott alisema lilikuwa jambo la kushtua sana kwamba wananchi wasio na hatia kutekwa nyara na mtu ambaye alikuwa anashinikizwa kisiasa.
Makomando walifyatua risasi na kisha kuingia ndani ya mgahawa huo huku wakirusha magurunedi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*