MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MKOANI MBEYA

MATOKEO ya awali yaliyopatikana  mkoani Mbeya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuongoza  katika maeneo mengi kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumzia matokeo ya awali,Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya alisema mpaka anazungumza na waandishi wa habari,matokeo yalipatikana kwenye vitongoji 2047 kati ya 2567, vijiji 606 kati ya 771 na mitaa 252.
Alisema  kwa upande wa vijiji vya Wilaya ya Chunya yenye vijiji 86 yalikuwa yamepatikana matokeo ya vijiji 74, ambapo  kati ya vijiji hivyo,CCM ilikuwa imeshinda vijiji 67 na Chadema vijiji saba.
Wilaya ya Ileje yenye jumla ya vijiji 71 ambapo matokeo yalikuwa yamepatikana ya vijiji 32 CCM ilikuwa imeshinda vijiji 23 na Chadema vijiji 9.
Kwa wilaya ya Kyela yenye jumla ya vijiji 93 ambayo matokeo ya vijiji vyote yalikuwa yamepatikana CCM imeshinda vijiji 79 na Chadema vijiji 13 huku kijiji kimoja uchaguzi ukiwa haukufanyika.
Wilayani Mbarali kuliko na jumla ya vijiji 102, matokeo yalikuwa yamepatikana ya Vijiji 97 ambapo  CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 81 na Chadema vijiji 16 na vijiji vitano yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya ya Mbozi yenye vijiji 125 ambapo matokeo ya vijiji 92 yalikuwa yamepatikana CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 84,Chadema vijiji  8 na vijiji 33 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya ya Rungwe yenye vijiji155,matokeo ya vijiji 150 yalikuwa yamepatikana,CCM ilishinda vijiji 127,Chadema vijiji 22,CUF kijiji kimoja na vijiji vitano matokeo yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya ya Momba ina vijiji 72 kati ya hivyo vijiji 67 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 43,Chadema vijiji 24 na vijiji vitano yalikuwa yanasubiriwa.
Kwa upande wa Mitaa Mbeya mjini kuliko na mitaa 181,CCM imeshinda mitaa 106,Chadema mitaa 71 na Nccr Mageuzi mtaa mmoja wakati katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba ulio na mitaa 71 Chadema iliibuka kidedea katika mitaa 46 na CCM ikaambulia mitaa 25.
Kwa upande wa Vitongoji,Chunya yenye vitongoji 438 ambapo matokeo ya vitongoji 288 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 270 na Chadema vitongoji 18.
Kyela yenye vitongoji 469 CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 377 na Chadema vitongoji 88 huku vitongoji vinne uchaguzi ukiwa unapaswa kurudiwa.
Wilaya ya Mbozi yenye jumla ya vitongoji 664 ambayo matokeo ya vitongoji 414 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 359,Chadema vitongoji 55 na matokeo ya vitongoji 250 yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya ya Rungwe yenye jumla ya vitongoji 694,matokeo ya vitongoji 634 yalikuwa yamepatikana na CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 557,Chadema vitongoji 110,Cuf vitongoji viwili na TLP kitongoji kimoja na vitongoji 60 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya ya Momba ina jumla ya vitongoji 302 kati ya hivyo vitongoji 242 matokeo yalikuwa yamepatikana ambapo CCM ilikuwa imeshinda 189,Chadema 53 na vitongoji 60 vilikuwa bado matokeo yakisubiriwa.
Mwisho.
Na Mbeya yetu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.