MATOKEO YOTE MISS WORLD 2014

Miss World 2014, Rolene Strauss aliyeiwakilisha South Africa akifurahi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014. 
Leo December 14 kwenye Historia ya mwaka 2014, Mashindano makubwa ya Miss World 2014 yalikuwa yakifanyika London, Uingereza ambapo washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Tanzania, Happiness Watimanywaakiwa mmoja ya washiriki hao. 
Mpaka leo asubuhi matokeo ya kura ambazo zilikuwa zikipigwa na watu zilimuweka mwakilishi huyo kuwa katika nafasi ya pili, akitanguliwa na Miss Thailand ambapo iwapo Happiness angekuwa namba moja basi ilikuwa moja kwa moja aingie kwenye Top 10 ya mashindano hayo. 
Kutokana na Hapiness kupitwa kura na Miss Thailand hakufanikiwa kuingia kwenye Top 10, huku katika wale waliotajwa ni wawakilishi wawili pekee, mmoja wa South Africa na mwakilishi wa Kenya waliofanikiwa kuingia Top 10. 

Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.