MSHINDI WA PROMOSHENI YA TUTOKE NA SERENGETI AZAWADIWA BAJAJI

 Meneja Mauzo  wa Serengeti Breweries Ltd  Mkoa  wa Morogoro Bw.Moses Bartazary (Mwenye kofia ) akikabidhi Funguo ya Bajaj Limo yenye uwezo wa kubeba abiria saba kwa  mshindi  wa kwanza wa shindano  la Tutoke  na  Serengeti  Bi Rukia Almas ambaye ni mkazi wa Kihonda na mfanyakazi  katika Bar ya  Kambarage iliyopo manispaa  ya  Morogoro





UJASIRI ULIVYO TENGENEZA MAISHA YA USHINDI KWA MAMA WA NYUMBANI

Kwa miaka kadhaa, Rukia
Almasi, mkazi wa Morogoro amekuwa akizongwa na uvumi kwamba kushiriki promosheni za bahati nasibu ni kupoteza muda, na kwamba ushindi mara nyingi unakua umepangwa.  Kwa kutozingatia mawazo na maono hayo ya watu wengi ndiko kuliko mfanya Rukia wa leo kujivunia kumiliki Limo Bajaji ya Serengeti ambayo ina uwezo wa kubeba watu saba kwa mkupuo.

Rukia ambaye ndiye mshindi wa kwanza wa promosheni ya Tutoke na Serengeti mwenye umri wa miaka 41 ni mtalaka na mama wa nyumbani anayeishi na watoto wake wawili na mtoto wa dada yake huko Kihonda Morogoro. Tangu atengane na mumewe Rukia anasema aliamua kuhamia Kihonda na kuweka makazi yake huko kwani gharama ya maisha ni nafuu.
“Baada ya kutengana na mume wangu maisha hayajawa rahisi. Nilisongwa na huzuni na mara kwa mara nilikuwa nikitafakari mambo yatakuaje mbeleni, kwa kuwa sikua na kipato maalumu wala kazi ya kudumu”…alisema Rukia.
Hata hivyo Rukia anasema amekua akijishughulisha na biashara ndogondogo ili kuweza kuingiza chochote. Wiki iliyopita, Rukia alitangazwa mshindi wa Limo Bajaji wakati wa droo ya kwanza ya promosheni inayotambulika kama ‘Tutokena Serengeti’.
Akiongelea jinsi gani alivyoibuka mshindi wa Limo Bajaj Rukia anasema “Kwa jinsi nilivyokuwa nashiriki nilikuwa kama najaribu vile, siku jihesabia kama na mimi naweza kuwa mshindi…baada ya kuibuka mshindi nilikuja kugundua kwamba kuishi na ule uvumi wa kwamba ushiriki wa promosheni hizi ni kupoteza muda, na kwamba ushindi si halali, ilikuwa ni kosa kubwa ambalo nimewahi kulifanya katika maisha yangu.
“Baada ya kushinda bajaji hii, nina uhakika kwamba maisha ya familia yangu yatakuwa mazuri kwa sasa, nilichopanga ni kuitumia kufanya biashara ya usafiri na natumai kipato tutakacho pata kitakidhi mahitaji mengi muhimu. Shukrani zangu za dhati ziende kwa Serengeti kwa kweli na napenda kuwahasa watu wote tuchangamkie fursa ambazo zinajileta mbele yetu kama mimi nilivyofanya kwenye hii ya ‘Tutokena Serengeti,” aliongeza Rukia.
Kwa mara ya kwanza, Rukia alianza kusikia habari njema kuhusiana na promosheni ya Tutoke na Serengeti kupitia redio akiwa na wenzake wakipata vinywaji. “Baada ya kusikia tangazo lile, niliamua kwa ujasiri na kuamini kwamba nitashinda bajaji na punde nilianza kuchukua hatua stahiki. Niliagiza bia zaidi, chapa ya Serengeti, na kuanza kutuma tarakimu zilizo kuwa chini ya kizibo kwenda kwenye namba 15317. Nililirudia zoezi hili pindi nilipopata nafasi ya kufanya hivyo.
Wiki iliyopita, Rukia alikuwa akitazama TV huku akipata kifungua kinywa na familia yakeambapo namba mpya ikajitokeza katika kioo cha simu yake huku akipiga hesabu huenda  ikawa simu ya kudaiwa deni. Alipopokea na baada ya salamu, sauti ya kiume ilisikika ikimpongeza kwa ushindi. “Kwanza sikuamini nikidhani ananitania lakini nilipoona anasisitiza kwa ujasiri, ndipo nikaamini ni kweli nilikua nimeshinda. Kwa kweli nilifurahi sana”….alisema Rukia.
Kampeni hii inatoa fursa kwa kila mtanzania aliye na umri wa miaka 18+ kushiriki na  kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo fursa ya kukuza utalii wa ndani kwa kumpeleka mshindi kufuurahia mapumziko mazuri ya mwisho wa wiki katika hifadhi za taifa, Limo Bajaj sita za kushindaniwa ambazo zina uwezo wa kubeba abiria saba kwa mkupuo. Ushindi wa pesa taslim zenye thamani ya milioni 100/= ambazo zimegawanywa katika makundi y ash. 5000, punguzo la bia sh 300 kwa bia ya Serengeti Premium Lager na bia za bure ambazo mtu atapewa baa yoyote ile nchini au kwa mawakala.
Ili kufanikisha kampeni hii, kampuni ya SBL imeungana na B-Pesa, wataalamu wa teknolojia  mpya ambayo hivi karibuni walizindua huduma mpya ya usafirishaji wa fedha ambao watahusika katika kusambaza fedha katika simu za washindi watakao patikana kokote nchini.
Jinsi ya kushiriki ni rahisi sana ambapo unachotakiwa kufanya ni kununua  bia ya Serengeti Premium Lager na angalia chini ya kizibo ambapo utaona namba za kuijiunga kwenye droo na utume kwenda SMS namba 15317. Kumbuka jinsi unavyoshiriki zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi za kushinda.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.