TAARIFA KAMILI YA BOMU LILILOLIPULIWA SONGEA NA KUUA MLIPUAJI

Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akitoa
maelezo kwa DCP Diwani Athumani ambaye aliwasili mkoani humo jana
kwaajiri ya bomu la kutengenezwa kienyeji ambalo askari wa doria
walinusurika kurushiwa na kumlipukia mlipuaji wa bomu hilo ambaye
alifariki papo hapo.


Askari WP Mariam mwenye namba 8616 akiwa amelazwa wodi ya
majeruhi hospitali ya Mkoa baada ya kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye
bega baada ya vipande vya bomu kumfikia akiwa na askari wenzake kwenye
doria siku ya sikukuu ya krisimas.

  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiuangalia mwili wa
mtuhumiwa wa ulipuaji wa bomu ambaye alitaka kuwarushua askari wa
doria wakati wa sikukuu ya krismas kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. (PICHA NA AMON MTEGA ,SONGEA)
-----------------------------------------

 NA AMON MTEGA,SONGEA
JESHI la Poilisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na timu ya makachelo
toka makao makuu ya jeshi hilo wanawasakaka watu watatu ambao
wanasadikiwa kujihusisha na ulipuaji wa mabomu huku mwenzao mmoja
akiwa amefia katika eneo la tukio baada ya kutaka kufanya jaribio la
kuwatupia  bomu bomu askari waliyokuwepo doria katika sikukuu ya
Krisimas ambalo lilimshinda na kumlipukia mwenyewe na kusababisha
kupoteza maisha papo hapo huku utumbo ukiwa umemwagika nje na  mkono
wake wa  kushoto ukiwa umekatika kabisa na vipande vyake hajijulikani
vilipo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa
jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna wa jeshi la Polisi,
kaimu mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jina nchini (DCP)  Diwani
Athumani alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1.30
usiku huko katika mtaa wa Kotazi uliopo kata ya Majengo manispaa ya
Songea ,timu ya askari wakiwa doria kulitokea mlipuko wa kitu
kinachozaniwa kuwa ni bomu ambalo limetengenezwa kienyeji  na
kusababisha kuwajeruhi  askari wawili .
DCP Athumani aliwataja askari waliojeruhiwa kuwa ni PC Mselem mwenye
namba G 7903 ambaye alijeruhiwa mkono wake wa kushoto na alitibiwa na
kuruhusiwa na  mwingine PC Mariam mwenye namba WP. 8616 ambaye
amejeruhiwa kwenye bega la mkono wa kushoto na amelazwa katika
hospitali ya Mkoa Songea(HOMSO)akiendelea kupata matibabu.
 Alisema kuwa timu ya makachelo toka makao makuu wakishirikiana na
makachero wa Mkoa wa Ruvuma wamejipanga vizuri kuhakikisha watuhumiwa
watatu waliohusika na tukio hilo pamoja na kufuatilia mtandao wake wa
hualifu wanakamatwa mara moja  kwani vitendo vya ulipuaji wa mabomu
umekithiri nchini ikiwemo Mkoa wa Ruvuma kwani hadi sasa ni tukio la
tatu kwa mwaka huu.
DCP Athumani alieleza zaidi kuwa wahalifu hao watakamatwa kirahisi
kutokana na tukio walilolifanya baada ya mwenzao kulipukiwa na bomu
hilo na kusababisha kifo chake walijaribu kutorosha mwili wa mwenzao
ili kupoteza ushahidi lakini ilishindikana baada ya askari polisi
doria wengine kuwahi eneo la tukio na wahalifu hao waliacha mwili wa
mwenzao na kutokomea kusikojulikana.
“Wahalifu hao waliuvuta mwili wa mwenzao kutoka katika eneo la tukio
kwa umbali wa mita zisizopungua 80 na 90 kwa lengo la kutaka kupoteza
usahidi  lakini waliwahiwa na askari wengine wa doria na kuuacha mwili
na kutokomea kusikojulikana” alisema DCP Athumani.
Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa
dini,wanasiasa,wazee, makundi mbalimbali  ya kijamii pamoja na
waandishi wa habari kuwa kitu kimoja katika kuwafichuwa waharifu hao
ili matukio hayo yasiweze kujirudia tena hususani Mkoa wa Ruvuma.
 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyetembelea
eneo la tukio na kuzungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko
makubwa alisema kuwa waharifu hao wanaishi kwenye jamii inayotuzunguka
hivyo ni vyema kila mmoja akaliona jambo hili kwa umuhimu wake wa
pekee kulipa uzito na kuwafichuwa wahalifu ili Mkoa uendelee kuwa na
amani kwani linaleta taharuki kwa jamii jambo ambalo linarudisha nyuma
shughuli za maendeleo.
 Naye Mganga Mkuu mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dkt. Benedkto
Ngaiza amethibitisha kupokea mwili mmoja  wa mtu ambaye amekufa ukiwa
utumbo umetoka nje na  majeruhi wawili ambao ni askari na kwamba
askari mmoja alitibiwa jana na kuruhusiwa huku mmoja akiwa amelazwa
wodi ya majeruhi namba mbili  akiendelea kupatiwa matibabu na hali
yake inaendelea vizuri.
CRT: DEMASHO.COM

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA