TBL YATOA SH. MIL 18 ZA KUSAIDIA KUKARABATI MIUNDOMBINU YA MAJI SOKO LA MACHINGA DAR

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akimkabidhi hundi yenye thamani ya sh. mil. 18.9, kwa  Mkurugenzi wa Kampuni ya Gotam General Traders, Winner Taluka (wa pili kushoto)  kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa miundombinu ya maji iliyoharibika baada ya Soko la Mchikichini Ilala  kuteketea kwa moto. Wanaoshuhudia hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana, kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa soko hilo, Rehema Matali,  Mjumbe wa Kamati ya Maji  katika soko hilo, Christopher Mbowe pamoja na Kaimu Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala, Ulinyelusya Mwamtobe.
 Kilindo akikagua kisima cha maji ambacho miundombinu yake iliharibika baada soko hilo kuteketea. Kisima hicho cha maji awali kilijengwa kwa msaada wa TBL.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto),  akiangalia chemba ambamo kuna pampu ya maji iliyoharibika wakati wa janga la moto lililoteketeza Soko la Mchikichini Ilala, Dar es Salaam, ambapo jana kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa sh. mil. 18.9 za kukarabati miundombinu ya maji katika soko hilo lenye wafanyabiashara wanaokadiriwa 7000.
 Kaimu Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala, Mwamtope akitoa shukurani kwa TBL kwa msaada huo wa kukarabati miundombinu.
 Kilindo 9wa pili kulia) akijadiliana jambo na  Rehema Matali kuhusu kalo linalotumiwa na Mama Lishe, Baba Lishe  kuoshea vyombo
 Moja ya mabomba yaliyoharibika na kutakiwa kufanyiwa matengenezo
Kilindo akitoka kukagua miundombinu ya maji katika soko hilo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*