Tuzo za Bodi Bora Katika Sekta ya Kibenki na Bima kufanyika mwezi ujao

 Mratibu wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, Bi Neema Gerald (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo pamoja na wawakilishi kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Matthew Kasonta (wa pili kushoto), na Bw. Kassim Malela (kushoto).
Bw. Matthew Kasonta (katikati), mwakilishi kutoka Capital Plus International (CPI) ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja kati ya wadhamini wa tuzo, Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald (wa pili kulia) na mwakilishi kutoka Capital Plus International (CPI) Bw. Kassim Malela (kushoto).  

TUZO za Bodi yenye Uongozi Bora ijulikanayo kama Best Board Leadership Award (BBLA), ambazo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wagurugenzi katika sekta ya kibenki na bima, zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi ujao. BBLA iliyopangwa kufanyika mwezi Januari tarehe 30 na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini, inaandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa BBLA Bi. Neema Gerald alisema tuzo hizo zinatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam.
Wadhamini wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Capital Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media, wakati wadhamini wengine wakiaswa kujitokeza zaidi kuunga mkono tuzo hizo.

"Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakuwazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.

Bi. Neema alisema kuwa utamaduni unaojulikana ni kuwa ni Maafisa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi Wakuu pekee ndiyo wanaothaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au jamii nzima kwa ujumla. "Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema. Alibainisha kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.
Tathmini hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya Wakurugenzi katika suala la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kuiongoza dira ya taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa hatua madhubuti na  utendaji wake.

Alitaja maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.
Aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka nchini wakati ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa na kujitokeza kwa makampuni mengi ya bima na masoko zaidi kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.
"Kwa mabadiliko haya wakati huu, hasa katika sekta ya fedha ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na mabenki zimekuwa zikifungua biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema, na kuongeza:
"Hili litafanikiwa tu endapo kampuni hiyo ya bima au benki itaendelea kufanya kazi kwa mafanikio. Kwa maana hiyo, bodi ya wakurugenzi itakuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha kampuni hiyo haifi, "alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA