HATIMAYE
wanaume waliobadirishana wake zao wakazi
wa kijiji cha Ndala kata ya Kandete,
Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe, Mbeya wafumaniana tena
na mmoja wao kupigwa faini ya kulipa ng’ombe wawili ikiwa ni fidia ya kukutwa na mke wa mtu.
Wanaume
hao ambao ni marafiki walioshibana walikuwa wakiibiana wake ambapo kila mmoja
alikuwa akichepuka na mke wa mwenzie ambapo juzi walifumaniana wakitoka kwenye
korido ya nyumba ya kulala wageni iliyopo kijijini humo.
Ilikuwa
patashika nguo kuchanika baada wa watu hao kushikwa na mshangao wakitukea
vyumbani huku kila mmoja akiwa amemkumbatia mke wa mwenzie na katika vurumai
wasamalia wema waliwapeleka katika serikali ya kijiji.
Baada
ya kufika kwenye ofisi ya afisa mtendaji wakajikuta wote wana makosa na ndipo
walipoamua kubadirishana wake zao na kuandikishana na kutia sahihi kwenye ofisi
hiyo kuwa kila mtu aendeleekuwa na mke wa mwenzie.
Baada
ya kufikia muhafaka huo mbele ya afisa mtendaji wa kijiji hicho Anna Lutengano
kila mmoja akaelekea nyumbani kwake akiwa na mke wa mwenzake wakiwa wamepeana
uhalali wa kuwamiliki.
Siku
mbili zilizopita afisa mtendaji huyo alishikwa na butwaa baada ya kuletewa kesi
ya watu hao kuwa wamefumaniana tena ambapo Poul Pomboma alifumaniwa
akijivinjari na Lusia Luswepo ambaye ni mke wa Ambakisye Mwakasege.
Kwa
mujibu wa afisa mtendaji huyo Anna Lutengano ni kuwa kijana Poul wakati wa
kubadirishana wake alikuwa bado anaupendo na mke wake na ndiyo maana akaamua
kumyemelea na kwenda nae kujivinjari na hatimaye akafumaniwa.
Afisa
huyo alisema kuwa baada ya kijana huyo kufumaniwa na mke wa mtu ambaye alikuwa
mke wake kabla hawajabadirishana alikiri na kutozwa faini ya kulipa ng’ombe
wawili na kulipa faini ya kuendeshea kesi.
Akisimulia
mkasa huo mhanga wa tukio hilo Poul Pomboma alisema huenda mwanamke huo
na hawala yake waliandaa mtego wa fumanizi hiyo kwa lengo la
kujipatia kipato na kuwa anajutia kufanya kitendo hicho.
Wananchi
kwa upande wao wamelani kitendo hicho na kusema
watakuwa msitari wa mbele kupinga na kukemea
vitendo hivyo na kwamba wanatarajia kumwandikia
barua mtendaji wa kijiji hicho kwa lengo la
kuwafukuza vijana hao katika kijiji hicho kwa madai kuwa wanawadharirisha.
Mwisho.
Comments