DORIS MOLLEL KATIKA UZINDUZI WA BWENI LA KWANZA KWA WATOTO WA JAMII YA HADZABE, SINGIDA


Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati alipohudhuria kwenye hafla ya ufunguzi wa bweni jipya maalum kwa watoto wa jamiii ya hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilaya ya Mkarama mkoani Singida. Uzinduzi wa bweni hili ni matunda ya jitihada za Serikali ya wilaya hiyo na mkoa wa Singida kuwahamasisha watoto hao kuhudhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya Ndg Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (Wa kwanza kushto).
Mlezi wa watoto wa jamii ya Hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilayani Mkarama mkoani Singida akimpongeza Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel baada ya kumteua kuwa ‘balozi wa elimu’ wa watoto wa jamii ya Hadzabe kwenye shule hiyo. Doris ambaye ni Miss Singida na Kanda ya Kati 2014/15 alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na mkuu wa Wilaya Ndg. Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (mwenye suti nyeusi).
Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel akikabidhi Blanketi kwa watoto wa jamii ya Hadzabe waliojengewa Bweni na Serikali ya Wilaya na Mkoa wa singida katika shule ya msingi Munguli Wilayani Mkarama ikiwa ni jitihada za Serikali kuwahamasisha kuduhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Akishuhudia tukio hilo ni Dk. Paseko Kone, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA