KATIBU MKUU WA CCM AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYA YA MJINI ZANZIBAR

      

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Balozi Ali Karume huku wakifurahia jambo mara baada ya kuwasili kwenye shehia ya Miembeni jimbo la Kikwajuni  wakati alipofika katika shehia hiyo kukagua mradi wa ukarabati wa zahanati ya (Nyumba ya Yasu)Miembeni,Kinana yuko katika ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar akikagua  utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, NEC CCM Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- ZANZIBAR) 2Katibu Mkuu wa CCM NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  kushoto akifurahia jambo na  na Balozi Ali Karume huku wakati walipokutana  katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanana mjini Zanzibar. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ukarabati wa zahanati ya Nyumba ya Yasu Miembeni wakati alipokagua ukarabati wa zahanati hiyo katika jimbo la Kikwajuni. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua jengo la maduka ya kasas ya  Shehia ya Vikokotoni  wakati alipotembelea mradi huo leo. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya utandazaji wa mradi mkubwa wa maji katika jimbo la Kikwajuni. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza maelezo ya wanafunzi mbalimbali wa kituo cha vijana Tanzania Youth Icon Mwembe Madema wakati alipotembelea kituo hicho kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki upishi wa Piza wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya vijana chaTanzania Youth Icon Mwembe Madema 8Hili ndiyo jengo la Kitegauchumi la maduka ya kisasa shehia ya Vikokotoni jimbo la Mji Mkongwe. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka mara baada ya kuzindua mradi wa maduka katika jengo la kitega uchumi cha shehia ya Vikokotoni jimbo la Mji Mkongwe. 10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekezwa jambo na mwalimu wa sanaa ya makaratasi Abdalah Suleiman  wakati alipotembelea kituo cha mafunzo kwa vijana cha Tanzania Youth Icon (TAYI) 11pMkuu wa mkoa wa Mjini Mh. Abdallah Mwinyi akizungumza na kushukuru Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Masauni Yusuf Masauni kwa kazi nzuri anayoifanya kutekeleza ilani ya CCM wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh. Vuai Ali Vuai wakati alipokuwa akitoa salam zake katika kituo hicho kushoto ni Abdallah Miraji Othman Mkurugenzi wa kituo hicho. 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mjini Ndugu Silima Borafya wakati alipokuwa akimkaribisha ili kuzungumza na wananchi kushoto ni Abdallah Miraji Othman Mkurugenzi wa kituo hicho. 14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya vijana cha  Tanzania Youth Icon jimbo la Kikwajuini mjini Zanzibar. 15Baadhi ya  vijana na wananchi wakiwa wamekusanyika katika kituo hicho. 16Umati wa vijana na wananchi wakimsikiliza Kinana. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha fedha jumla ya shilingi milioni mbili zilizokabidhiwa kwa mkurugenzi wa Kituo cha Vijana cha Tanzania Youth Icon. 19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Masauni Yusuf Masauni wakati akikabidhi baiskeli kwa mwasheha wa jimbo hilo. 21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinawa maji pamoja na Diwani wa Nasoro Salim Maarufu kama Arjazeera, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa CCM NEC Itikadi na Uenezi. 24Mbunge wa jimbo la Dr. Hussein Mwinyi akishiriki kazi za kuchimba na kutandaza mabomba ya maji Mkunguni katika jimbo la Kwahani. 25Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa Mkunguni kabla ya kuzindua mradi wa maji. 26Mbunge wa jimbo la Dr. Hussein Mwinyi akizungumza na wapiga kura wake tawi la Mkunguni. 27Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi jezi kwa vijana wa jimbo la Jang’ombe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI