KINANA AFANYA ZIARA ZANZIBAR KATIKA MAJIMBO YA BUBUBU, DOLE, MFENESINI NA MTONI

 Kinana akiongoza kupanda miti katika  shamba la  viungo vya vyakula la Spice Solution,Jimbo la Mfenesini, Zanzibar leo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Zanzibar. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiangalia Vanilla alipotembelea shamba la Spice Solution katika Jimbo la Mfenesini, wakati  wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inaotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM
 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa  Ushirika wa Shamba la viungo vya vyakula la Spice Solution Farm eneo la Mwakaje, Othman Abdul Mohamed alipotembelea shamba hilo wakati wa ziara yake katika  Jimbo la Mfenesini, Zanzibar
 Kinana akiwa amevalia kofia na tai za mapakacha baada ya kutembelea shamba la viungo mbalimbali vya vyakula la Spice eneo la Mfenesini.
 Kaimu Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Mjini Magharibi, Salama Abbas Kaboyonga akiangalia pilipili zenye rangi nyeusi, nyekundu na nyeupe katika shamba la Spice Solution wakati wa ziara ya Kinana katika Jimbo la Mfenesini.
 Kinana akishirikiana na Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha kujenga jengo la CCM Tawi la Bububu, Wilaya ya Mfenesini, Zanzibar

 Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Kijichi, Jimbo la Bububu, Zanzibar
 Mbunge wa Jimbo la Dole, Zanzibar, Silvester Mabumba akielezea utekelezaji wa miradi katika Jimbo hilo. Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
 Kinana akiwa amezindua rasmi gari la kubebea wagonjwa  lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dole kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa jimbo hilo.
 Kinana akifukia bomba la maji wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Mbuzini, Jimbo la Mfenesini Zanzibar
 Kinana akimtwisha ndoo ya maji Khadija Isa Kibwan baada ya kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mbuzini, Jimbo la Mfenesini, Zanzibar.
 Kinana akiangalia viungo mbalimbali vilivyotengenezwa katika shamba la viungo la Spice Solution
 Pilipili zenye rangi tofauti zinzozalishwa katika shamba la Spice Solutions Jimbo la Mfenesini, Zanzibar

 Kinana akimvisha mtoto nguo aliyoinunua alipokuwa akikagua kazi za kikundi cha akina mama cha Mwenye kusubiri hachoki, katika Tawi la Mtopeka, Jimbo la Mtoni.
 Akina dada wafuasi wa CCM wakiimba utenzi wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Geji, Jimbo la Bububu, Zanzibar.
 Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha akihutubia katika mkutano wa hadhara uliotubiwa pia na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Geji Jimbo la Bububu, Zanzibar jana, ambapo aliwataka wananchi kuipigia kura Katiba inayoyopendekezwa Aprili 30, mwaka huu.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo
 Mtoto wa Mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Abeid Amani Karume, Ally Karume akihutubia katika mkutano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Geji, Bububu Zanzibar, ambalo aliisikitikia CUF kukubali kuungana kwenye UKAWA Chadema chama ambacho awali kilikataa kuungana nacho kuunda kambi ya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.