KINANA AMPONGEZA DK.SHEIN KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO ZANZIBAR

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki pamoja na wananchi kujenga tuta la kuzuia maji chumvi kuingia kwenye mashamba ya mpunga ya Koowe, wakati wa ziara yake wilayani Micheweni, Pemba ya kuimarisha uhai wa chama  na kukagua mikradi mbalimbali inayotekelezwa kwa kufuta Ilani ya Uchaguzi ya CCM YA MWAKA 2010.
 Komredi Kinana akilakiwa na wananchi alipowasili katika Bonde la Mpunga la Koowe, kushiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi kuingia kwenye bonde hilo.Kinana alisifu juhudi la Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa visiwa vya Pemba na Unguja.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Kinana akipata maelezo kuhusu ujenzi wa tuta hilo kutoka kwa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Dk. Suleiman Shehe Mohamed.
 Kinana akiondoka baada ya kushiriki ujenzi wa tuta hilo.
 Komredi Kinana akilakiwa na wananchi alipowasili Mnarani Makangale kushiriki ujenzi wa Maskani ya Vijana ya CCM waliovihama vyama vya CUF na ADC.

 Kinana akishiriki ujenzi wa maskani hiyo.
 Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni, wakisalimiana na Komredi Kinana alipowasili kukagua wodi mpya ya kulaza wagonjwa na ujenzi wa chumba cha upasuaji hospitalini hapo.


 Komredi Kinana akikagua  wodi mpya katika Hospitali ya Micheweni.
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni.
 Komredi Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Majenzi mjini Micheweni leo.
 Mbunge wa CCM Viti Maalumu, Maua Daftari, akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwataka wazanzibar kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa kwani imejali manufaa yao, likiwemo suala la mafuta na Nishati kuwa mali ya Zanzibar, Kujiunga na Taasisi za Kimataifa, Mzanzibar kumiliki ardhi Tanzania Bara.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwataka wananchi wakiwemo wapinzani kuyakubali maendeleo yaliyoletwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tangu 1964, ambapo zimejengwa barabara, maji, vituo vya afya na majengo na Micheweni kuipa hadhi ya wialaya mwaka 1964.
 Wananchi wakinyoosha juu mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuipigia kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa ambayo imekuwa na manufaa mengi kwa wazanzibar
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa  Hamad Mberwa akihutubia katika mkutano huo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara, kwenye Uwanja wa Majenzi mjini Micheweni, Pemba, ambapo aliwataka wananchi na wafuasi wa CUF,kuachana na tabia ya woga ya kuwahoji viongozi wa CUF wakiwemo wabunge na wawakilishi ambao wamechukua majimbo yote Pemba, fedha wanazopata za maendeleo ya jimbo jumla sh. mil 40 kwa jimbo kila mwezi wanazipeleka wapi? kwani hawazitumii kupeleka maendeleo katika majimbo badala yake wanazitumia kwa maslahi yao binafsi. Wakati wabunge wa NA WAWAKILISHI WA ccm wameundiwa kamati za kuhakikisha fedha hizo za jimbo zinatumika kwa maendeleo majimboni.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA