Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mohamed Asenga Akifungua kikao cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki ,kulia kwake ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya Sitalike Slivester Nswima na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Said Juma Maraba.
Wataalam wakifuatilia kwa umakini mjadala wa kikao cha madiwani Halmashauri ya Nsimbo
(Picha na Kibada Ernest-Katavi)
……………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada –Katavi
Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameshauriwa kupima Afya zao na hasa maambukizi ya VVU kabla ya kuchukua fomu za kugombea Udiwani kwenye Kata zao ili waweze waweze kuwa mfano kwa watu wanaowaongoza na kutambua afya zao kama kweli watakuwa na nguvu za kutosha kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa kipindi cha kuwepo madarakani.
Diwani wa Kata ya Kapalala Reward Sichone alitowa ushauri huo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Nsimbo baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya kamati ya kuthibiti ukimwi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa hiyo Diwani wa Kata ya Sitalike Silvester Nswima.
Diwani Sichone alieleza kuwa ni vizuri kwa madiwani hasa wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo wanao tarajiwa kumaliza muda wao mwaka huu wakaandaliwa utaratibu na Halmashauri wa kupimwa maambukizi ya VVU kabla ya kumaliza muda wao wa uongozi mwaka huu ili waweze kuwa mfano kwa watu wao wanao waongoza.
Alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa endapo watapimwa afya zao mapema itawafanya wajitathimini kabla ya kuchukua fomu za kugombea udiwani.
Sichone alisema endapo diwani atapimwa na kukutwa anamatatizo kwenye afya yake itamsadia kuona kama kweli atakuwa na uwezo wa nguvu za kufanya kazi za wananchi kwenye eneo lake.
Alifafanulia kuwa haitakuwa vizuri kwa diwani ambaye atapimwa na kukutwa na maambukizi ya VVU halafu achukue fomu za kugombea tena wakati anajua kuwa hana nguvu za kufanya kazi za wananchi wake hivyo swala la madiwani kupima afya zao ni jambo la msingi sana
“Jamani mnacke lakini mambo haya ni muhimu sana katika jamii zetu hasa wananchi tunaowaongoza wakiona tunafanya namna hiyo wanakuwa na imani nasisi ingawa kupima siyo lazima ni hiari ya mtu “alisema Diwani Sichone.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti Ukimwi wa Baraza la Madiwani Sylvester Nswima ambae ni Diwani wa Kata ya Sitalike alipinga ushauri huo wa Diwani Sichone
Nswima alieleza kuwa swala la Madiwani kupimwa afya zao kwa pamoja haiwezekani kwani kupima ni hiyari ya kila mtu na sio lazima,hivyo kila mtu atapima kwa muda wake na kwa hiari yake.
Naye Mwenyekti wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alisema kitendo cha madiwani kupima afya zao kinaweza kuwa ni mfano mzuri kwa watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo kuona viongozi wao wakimwa afya na kuwafanya nao wataiga mfano wa kupima mara kwa mara afya zao.
Aliwatoa wasiwasi kwa kusema kuwa “Madiwani tusihofu kupimwa bali tuangalie utaratibu wa kuwaita wataalamu waje watupime afya ili tuwe mfano kwa watu wengine kwenye Halmashauri yetu na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake”alisema Mwenyekiti Mohamed Assenga.
Katika taarifa ya utekelezaji wa shughuli za ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa hiariwalifanikiwa kupima watu 1221 kati ya wanaume 668 na wanawake ni 551 ambapo kati ya watu hao waliopima waliokutwa na maambukizi walikuwa watu 36 kwa Halmashauri ya Nsimbo.
Comments