MBUNGE WA MOROGORO MJINI ATOA WIKI MBILI MTENDAJI WA KATA KURUDISHA FEDHA ZA WANANCHI

 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiongea Kwa Msisistizo Akimtaka Mtendaji wa Kata ya Luhungo Iliyopo Mzee Makame Kai Kurudisha Fedha za Wananchi wa Kata Hiyo Shilingi Milioni 1.4 Ndani ya Muda wa Wiki Mbili la sivyo atangulie Polisi.Mh Mbunge Ametoa Kauli Hiyo katika ziara yake aliyoifanya kata ya Luhungo Kwa jili ya Kusikiliza Kero za wananchi na Ndipo wakazi wa Kata Hiyo walipotoa Malalamiko kwa Mbunge wao Kuhusu Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata Hiyo Aliyefahamika kwa Jina la Mzee Makame Kai. Wananchi walimweleza Mbunge kuwa Mtendaji huyo amechukua fedha za Maendeleo ya Kata Hiyo Kinyume na Utaratibu na Alipotakiwa kuzirudisha amekuwa na Maneno Mengi Bila Kuzirudisha ia Kufuja Pembejeo za wakulima Ndipo Mbunge Abood Alipotoa kauli ya Kumshugulikia kwa Kumpa wiki mbili fedha za Wananchi ziwe zimerudi.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwasikiliza viongozi wa Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia Jumla ya Shilingi Milioni 2
 Wakazi wa Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro waliojitokeza Kumsikiliza Mbunge wao Mh Abood aliowatembelea Kusikiliza Kero zao Ambapo wakazi hao walilamikia Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata hiyo Mzee Makame Kaialiyefuja Fedha za Miradi ya Maendeleo Pamoja na Kuuza pembejeo za wakulima.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokea Taarifa za Chama Kutoka kwa Katimu wa CCM Kata ya Luhungo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akisikiliza kwa makini Kero Mbalimbali zinazowasumbua wakazi wa kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro sambamba akiwa na Diwani wa Kata hiyo kushoto Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lugala Kulia.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokea Taarifa za Maendeleo kata ya Luhungo Kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Kata Hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Kivuko Kinachounganisaha Mtaa wa Majengo na Mshikamano Eneo la Lukobe Kata Ya Kihonda Manispaa ya Morogoro wakati wa Mfululizo wa Ziara zake ya Kutembelea Kata Zinazounda Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Mbunge aliahidi Kujenga Kivuko Hicho mara baad ya Kutembelea Eneo Hilo na Ndipo wakati wa Eneo Hilo walipomwomba Mbunge wao Kuwatatulia Kero ya eneo hilo muhimu inayowaunganisha wakazi wa Mitaa hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Ujenzi wa Kivuko hicho ambapo Mpaka ujenzi utakapokamilika Utagarimu jumla ya Shilingi Million 6.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA