MRISHO MPOTO : FURAHA ILIYOJEE BAADHI YA MATAIFA KUTUMIA MUZIKI WANGU KAMA SEHEMU YA MASOMO KATIKA VYUO VYAO
Muziki wa Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ umezidi kupasua anga la
kimataifa na kubisha hodi katika mataifa mbalimbali kwa kutumika kama
sehemu ya masomo katika sekta za elimu ikiwemo vyuoni.
Msanii huyo ambaye ni balozi wa lugha ya kiswahili, ameshea
moja ya video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwaonyesha wanafunzi wa
chuo cha Wales kilichopo nchini Marekani wakijifunza somo la kuzuia na
kupambana na ujangilia kupitia video ya wimbo wake ”Deni la Hisani”
ambayo amemshirikisha Peter msechu kwenye kiitikio.
”Faraja iliyoje
baadhi ya mataifa duniani kazi zangu ni sehemu ya masomo katika vyuo
vyao, asante watanzania kwa kuendelea kunijenga kimataifa, #Njoouichukue
j3”, aliandika Mpoto kwenye mtandao wa Instagram
Comments