Mwanza walitaka Tamasha la Pasaka

      

imagesNa  Mwandishi Wetu
WAKAZI wa jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa  wameiomba Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa Tamasha la Pasaka na Krismasi  kuwapa  nafasi  ya upendeleo  kwa  kuwapelekea tamasha katika mkoa huo.
Sababu za kupewa kipaumbele katika Tamasha la Pasaka mwaka huu ni baada ya kulikosa Tamasha la Kirismasi ambalo lilifanyika kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa  na  Songea .
Kwa  mujibu  wa  wakazi hao ambao waliwaomba waandaaji wa matamasha hayo ya injili, Kassim Mtolea mwanafunzi  wa   Chuo cha SAUT wanamuomba Mkurugenzi wa Kampuni ya  Msama Promotions  Alex  Msama na kamati yake kuwafikiria kwa sababu  linashirikisha waimbaji wa Kimataifa.
Mtolea alisema  wanamuomba  Msama  kuwafikiria  zaidi  kwa  sababu  miaka  yote  tangu  limeasisiwa limekuwa likianzia jijini  Dar es Salaam hivyo ni vyema waandaaji wakabadilika na kulipeleka kwanza Jijini Mwanza.
Aniceth  Nyahore  ambaye  ni  mkazi  wa  Maswa  lalieleza kuwa iwapo tamasha hilo litaanzia Mwanza  litakutanisha  mikoa  ya  Geita,  Shinyanga,  Mara  na  Kagera   katika  uwanja wa CCM Kirumba  na kueneza injili pamoja na burudani.
 
Nyahore  alisema   ubora  wa  Matamasha  hayo unatokana  na  ushiriki wa waimbaji wa Kimataifa wanaotoka nchi za Afrika Kusini,  Kenya,  Uganda,  Rwanda  na  Uingereza ambao umekuwa ukivutia umati mkubwa wa mashabiki.
Daniel  Mkate  aliishauri Kamati ya maandalizi kuzingatia kuanza na mkoa wa Mwanza  baada ya kulikosa Tamasha la Krismasi lililofanyika mwaka jana huku wakazi hao wakiwa na kiu kubwa.
Sambamba  na  kuliomba  tamasha  hilo  mkoani   humo  pia  aliishukuru  Kamati  ya  Maandalizi  kwa  kumleta  muimbaji  Rebecca  Malope ambaye alishiriki tamasha la mwaka juzi.
Aidha Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alikiri kupokea maombi haya ambapo alisema ni vigumu kutoa maamuzi maana bado ni mapema mno, lakini aliahidi kuyafanyia kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI