RAIS KIKWETE AWASI|LI RIYADH KUHANI KIFO CHA MFALME WA SAUDI ARABIA, KUFANYA ZIARA YA KIKAZI UJERUMANI NA UFARANSA

      

 unnamedjkRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Januari, 2015

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA