RIDHIWANI KIKWETE KUTUMIA UANASHERIA WAKE KUTETEA HAKI ZA WANYONGE CHALINZE

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi mjini Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani jana, ambapo pamoja na kuwashuru kwa kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
 Ridhiwani akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Masoko mjini Chalinze
 Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
 Mkazi wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo.
 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze.
 Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao
 Ridhiwani akimsalimia mmoja wa wazee wa Kitongozi cha Chalinze Mzee
 Mmoja wa vijana wa Chalinze Mzee akiuliza swali
 Mzee Ibrahim Koga akielezea mbele ya Mbunge asivyotendewa haki na Baraza la Kata ya Bwilingu la kuporwa ardhi yake
Mama mwenye Jamii ya Kimasai Rehema Lazaro akilalamika mbele ya mbunge kitendo cha baadhi ya wananchi kutoa lawama kwa wafugaji wote badala ya wafugaji wanaofanya vurugu kwa kupeleka mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuchafua visima vya maji.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*