SINGANO AIVUSHA SIMBA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


SAM_4333

Kikosi cha Simba sc kilichoanza 
WEKUNDU wa Msimbazi wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Mapinduzi kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vinara wa ligi ya Zanzibar, JKU katika mechi iliyomalizika usiku huu uwanja wa Amaan Zanzibar.Bao pekee la Simba limefungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika dakika ya 11 kwa shuti kali  akipokea pasi murua ya Said Ndemla.
SAM_4332
Kikosi cha JKU kilichoanza 
Kwa matokeo hayo, Simba wameibuka vinara wa kundi C kwa kujikusanyia pointi 6 kibindoni, huku nafasi ya pili ikishikwa na Mtibwa Sugar wenye pointi tanoSimba walianza mchezo kwa kasi, lakini JKU walionekana kuchakarika kuwadhibiti wakali hao wa Msimbazi.Kikosi cha Mnyama kinachonolewa na Mserbia Goran Kopunovic kimeonekana kucheza mpira wa kasi na pasi za uhakika kuanzia sehemu ya ulinzi na safu ya ulinzi.Baada ya mechi hiyo, kocha Kopunovic amesema timu yake inaimarika kidogo kidogo na ilicheza tofauti kwa vipindi vyote.

“Hii ni siku ya tano tu tangu nifike, bado naendelea kuwapa mbinu mpya. Wachezaji wangu kimbinu nawaona wazuri”
“Mimi napenda vijana ndio maana nawatumia wengi. Kidogo kidogo tutakuwa safi” Alisema Kopunovic.
Simba wanasubiri mpinzani wao wa Robo fainali katika mechi za kesho ambapo kutakuwa na mechi nne.
Majira ya saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Amaan, KCC watachuana na KMKM, saa 11:00 jioni Azam fc watakabiliana na Mtende, hizo ni mechi za kundi B.
Kundi A, Taifa ya Jang’ombe itapepetana na Polisi katika uwanja wa Mao Dze Tung majira ya saa 9:00 alasiri.
Mtanange mwingine wa kundi A utawakutanisha Yanga dhidi ya Shaba majira ya saa 2:00 usiku uwanja wa Amaan.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI