Vijana jiwekeeni malengo kabla ya kukimbilia mikopo: Kongoye

       

unnamedMkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Christopher Ryoba Kangoye akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za maisha na ujuzi jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa Dodoma.
unnamedKijana Ramadhani Khalid kutoka Kikundi cha Umoja wa Vijana Ng’ambo (UVING’A) kilichopo Wilaya ya Mpwapwa kinachojishughulisha na ufyatuaji wa matofali akishindilia mchanga katika mashine ya kufyatulia matofali kuwaonyesha maafisa waliotembelea mradi wa kikundi hicho jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wapili kutoka kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
unnamed2 Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada ya Uongozi kwa vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma. unnamed3Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa wakifuatilia mada zilizokua zikitolewa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
unnamed4Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiangalia Cheti cha usajili wa Kikundi cha Wapakaya kinafanya kazi ya kutengeneza Pikipiki kilichopo Wilaya ya Mpwapwa walipowatembelea wanakikundi kwa ajili ya kukagua mradi wa wanakikundi hao. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Mpwapwa Bw. Paschal Jeremiah. unnamed5Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akishika jiko banifu linalotengenezwa kwa kutumia udongo mfinyanzi kuangalia ubora wa jiko hilo lililotengenezwa na wanakikundi cha Kujiamini kilichopo Wilaya ya Kongwa wakati wa kukagua miradi ya Vijana wa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma.
(Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)
…………………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutokimbilia mikopo inayotolewa kwa vijana kabla ya kujipanga na kuwa na malengo ya matumizi ya mikopo hiyo kwa maendeleo ya Taifa.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Christopher Ryoba Kangoye wakati wa ziara ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake na baadae kukutana na vijana wa wilaya hizo jana Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
“Vijana wamekua na tabia ya kukimbilia mikopo inayotolewa na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kabla ya kujipanga hivyo kushindwa kutumia fedha hizo kwa uangalifu na hatimaye kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati”, alisema Bw. Kangoye.
Aidha Bw. Kangoye amesema kuwa vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo wanapaswa kujitambua na kutumia nguvu hizo zitakazozalisha matunda mazuri kwani ili mtu aweze kuendelea lazima afanye kazi kwa bidii na kwa ufanisi.
Akizungumza kwa niaba ya maafisa kutoka Wizarani waliofika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa amesema kuwa Wizara inayosimamia masuala ya Vijana imepanga mikakati mingi ya kuwainua vijana wa taifa hili hivyo kuiomba Wilaya ya Mpwapwa kushirikiana na Wizara inayosimamia vijana kuwaongoza vijana wa Wilaya yao kuwa lulu ya taifa itakayomulika vijana wengine kutoka Wilaya zote nchini Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa Bw. Paschal Jeremiah amesema kuwa vikundi vya vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa vilipatiwa mkopo wa shilingi milioni 10 mnamo mwaka 2009 na urejeshaji wa mkopo huo umefanyika kwa asilimia 90 hali inayoonyesha kuwa vijana wa Wilaya yake wako makini na wanastahili kupatiwa mkopo mwingine kuendeleza shughuli walizozianzisha.
Naye kijana Briton Ivan Majele kutoka kikundi cha Umoja wa Vijana Ng’ambo kilichopo Wilaya ya Mpwapwa kinachofanya kazi ya kufyatua matofali amewataka vijana wenzake nchini kutobweteka bali wathubutu na kuamini kuwa mtaji mdogo unaposimamiwa vizuri huzaa na kuwa mkubwa hivyo kuthamini kile kidogo walichonacho na kukiendeleza.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI