WAKAZI WA TEMEKE NA VITONGOJI VYAKE WALIPOKEA VYEMA TAMASHA LA TUO8JANUARY, JIJINI DAR

  Hii
ilikuwa ni picha ya pamoja ya wasanii na mashabiki waliojitokeza kuunga
mkono tamasha hilo la bure ambalo lina lengo la kuhamasisha vijana
kushiriki katika maamuzi yenye mustakabali wa nchi.
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya
aina yake pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi
katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 
Wakiongowa na  Hamis
Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili, wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha
mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu
hiyo.
 
Akizungumza kabla ya kuimba
nyimbo zake kali,Mwana FA akitumia tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’,
aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na
kuchagua viongozi wanaowataka.
 
“Vijana wenzangu.., tusisubili
watu wengine watufanyie maamuzi.., ni sisi wenyewe tunatakiwa kuamua
tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu
unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema
Mwana FA.
 
Mara baada ya kusema hayo,
alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa sasa ukiwemo, mfalme ambao
uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani hapo.
 
Mbali nma Mwana FA, pia Niki wa
pili alipata mapoekzi makubwa viwanani hapo kwa nyimbo zake kali huku pia
akisisitiza vijana kuchakua maamuzi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Wanamuziki
wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni
pamoja na Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and kenzo, Dogo Janja,
Madee, Chegge, Temba, mwasiti na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya
mashabiki
waliojitokeza kuimba nao sambamba.
Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na
Morogoro ambapo linalengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na
kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika
Oktoba mwaka huu.
 
PICHANI
jUU:  Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza katika
tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga jana.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa
OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa
wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya
sabasaba jana jioni mjini Morogoro. 

 Mtayarishaji
nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk’ akichana
mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January lililofanyika
katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
 Baadhi
ya wakazi wa Temeke waliojitokeza kwenye onesho hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar hapo jana.
Wasanii
Chegge na Temba kutoka TMK Wanaume Family wakitumbuiza katika tamasha
la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga
 Mkali
mwingine wa kughani mitindo huru, Godzilla akitumbuiza jana jioni katika viwanja vya Mwembe Yanga,Temeke jijini Dar,kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika hapo jana.
Pichani
kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia
jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa
morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo
jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
Pichani
kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia
jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa
morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo
jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
 Wasanii
Aika, na Nahreel wanaounda kundi la Navy & Kenzo wakitumbuiza
katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya
MwembeYang,Temeke jijini Dar.
Baadhi ya wadau wakirekodi tukio muhimu
 Pichani Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka mbele ya mashabiki wake huku shangwe za mayowe na
vifijo zikiwa zimetawala uwanjani hapo  jana.
Wasanii
Madee na Dogo Janja ( hayupo pichani) wakitumbuiza katika tamasha la
Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini
Dar.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI