WANAFUNZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA BUFALO NA EMPIRE VYA MAREKANI WAWASILI NCHINI KWA ZIARA YA MAFUNZO


Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (katikati mwenye kofia)  akiwa na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Bufalo na Empire vya Marekani baada ya kuwapokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo. Wanafunzi hao wamewasili nchini kwa mwaliko wa mbunge huyo ambapo watatembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Jimbo lake pamoja na Kampuni yake ya Bravo Job Centre Agency LTD. Wageni hao watapata fursa ya kutembelea jimbo la Temeke, Rolya, Tarime, Kilimanjaro na Mara ambapo watajifunza mambo kadhaa na wataondoka nchini Januari 21, 2015. PICHA NA KHAMISI MUSSA
 Mbunge Mtemvu kulia, akielekeza jambo.
……………………………………………………………………………………………
Na Khamisi Mussa
WANAFUNZI 10 kutoka vyuo Vikuu vya Bufalo na Empire vya Marekani wamewasili nchini kwa ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu.
 Akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo mara baada ya kuwapokea wanafunzi hao ambao wanaongozwa na Profesa Dan Nyaronga, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu alisema wageni hao watapata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Jimbo lake pamoja na Kampuni yake ya Bravo Job Centre Agency Ltd.
Alisema mbali ya kutembelea jimbo la Temeke pia watatembea Taasisi ya Wajasiriamali ya Poverty Fighting Tanzania iliyopo Tandika na mkoa wa Mara, katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kitenga ambayo waliichangia sh.milioni 1.5, Miradi ya Maendeleo ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime Magharibi, Shule ya Bohare Community Development na Hospitali ya Mkoa wa Mara ambapo watajifunza masuala ya afya.
Alisema baada ya ziara ya mkoa wa Mara watatembelea mkoa wa Kilimanjaro na mbuga za wanyama na kuwa wataondoka nchini Januari 21, 2015.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*