ZIARA YA KUSHTUKIZA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALA JIJINI DAR


 Naibu Wazir wa Maji Waziri Makala akifuatana na wajumbe wa Bodi na Menejimenti, watendaji wa DAWASCO, waandishi wa habari na wananchi wa Boko wakati wa Ziara yake ya kushtukiza katika eneo la Boko jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya maeneo yenye matatizo ya maji ambayo yanasababisha wananchi wengi kukosa huduma hiyo muhimu katika masiha yao.
Naibu Waziri wa Maji Waziri Makala pamoja na wananchi wakishuhudia moja ya eneo ambalo linahusishwa na kuhujumu maji katika eneo la Boko mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO.
Naibu Waziri wa Maji Amos Makala ameiagiza Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya jiji la Dar es salaam (DAWASCO) kuviwezesha vitengo vya Habari na Biashara ili vifanye kazi karibu na wananchi.

Naibu Waziri Makala alisema hayo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua na kujionea namna miundo mbinu ya maji ya DAWASCO inavyohujumiwa na baadhi ya watu wachache na kuwakosesha wananchi waliowengi huduma muhimu ya maji katika maeneo yao wanakoendesha maisha yao ya kila siku.

“Kumekuwa na mawasiliano mabovu kati ya baadhi ya viongozi wa DAWASCO na wananchi, ni lazima mbadilike na kila mmoja atoe taarifa kwa wananchi ili wawe wanajua tatizo la wao kutokupata maji ni nini na litatatuliwa linatatuliwaje” alisema Makala.

Akizungumza na wakazi wa Boko jijini Dar es salaam, Makala alisema kuwa viongozi wanamaelezo mazuri ila hawana mawasiliano mazuri na wananchi pia wawe na lugha nzuri kwa wateja wao wanapofika ofisini kuhitaji huduma ya kuunganishiwa maji, kutoa kero zinazowasibu au tatizo la miundo mbinu ya maji kwenye maeneo yao inayosababisha upotevu wa maji mengi bila sababu. 

Aidha, wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri Makala aliwasimamisha kazi Meneja wa DAWASCO eneo la Boko Robert Mugabe na Meneja wa Kimara Peter Chacha na kuagiza Bodi na Menejimenti ya DAWASCO kuwapangia kazi nyingine na nafasi zao zijazwe mara moja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASCO alisema kuwa operesheni ya wahujumu maji Dar es salaam itakuwa ni endelevu, wale wote waliokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na sheria itachukua mkondo wake.

Ziara ya Naibu Waziri Makala akifuatana na wajumbe wa Bodi na Menejimenti, watendaji wa DAWASCO na waandishi wa habari ilianzia kukagua maeneo yenye matatizo maji ambayo yanapelekea wananchi kukosa maji ya maeneo mbalimnbali jijini Dar es salaam yakiwemo Mgomeni, Manzese, Boko na kuhitimisha ziara hiyo maeneo ya Kimara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI