Aleyekuwa mwenyekiti wa UVCCM na mjumbe wa NEC Ludewa afariki dunia

 Aliyekuwa MNEC  wa  wilaya ya  Ludewa  Elizabeth Haule  wa  pili kushoto enzi za uhai  wake  akiwa na viongozi  wa  wilaya  hiyo wakati wa mkutano mkuu wa wilaya ya  Ludewa mwaka jana ,kulia  ni mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ,aliyesimama ni mwenyekiti  wa CCM wilaya  ya Ludewa Stanley Kolimba na wa kwanza  kushoto katibu  wa CCM wilaya ya  Ludewa Eliud Semauye (picha na maktaba ya matukiodaimaBlog)
 
 
CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  wilaya ya  Ludewa  mkoani  Njombe  kimepata  pigo  kubwa kufuatia  kifo  cha  aliyekuwa  mjumbe  wa  Halmashauri  kuu ya wilaya  hiyo (NEC)  Bi  Elizabeth Haule.

Mbali ya  kuwa MNEC  wa  wilaya  hiyo  Haule  pia  alikuwa ni mwenyekiti  wa UVCCM wilaya ya  Ludewa  kabla ya  kujiuzulu kwake mwezi  February mwaka jana baada ya  kuchaguliwa nafasi hiyo ya  NEC na  nafasi   hiyo  kuwa  wazi  hadi sasa.

katibu   mwenezi  wa  CCM  wilaya  ya  Ludewa  Felix Haule  alisema  kuwa  kifo cha  kionozi  huyo  kimetokea  usiku  wa kuamkia leo akiwa katika  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa ambako  alilazwa jana  mchana kwa tatizo la  moyo.

Bw  Haule  alisema  kuwa siku ya  jumatatu wiki  iliyopita   marehemu  alipata   kuongoza  kikao  chake  cha mwisho   cha baraza la vijana  la  wilaya ya  Ludewa  na baada ya  hapo hali  yake ya afya  ilianza  kuzidi  kuwa mbaya  zaidi kabla ya kuamua jana  kwenda Hospitali ambako  walimlaza 

Alisema  kuwa mazishi ya  mjumbe  huyo wa NEC  wilaya ya  Ludewa yanataraji  kufanyika  kesho  kutwa jumamosi kijijini kwake Mholo kata ya Luana wilayani  Ludewa .

Kwa  upande  wake  mbunge wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akielezea  kifo cha  MNEC  huyo  alisema  kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya  kifo  hicho na kuwa kwa  sasa  anafanya maandalizi ya  kuelekea   jimboni  Ludewa  ili  kuungana na  wana CCM na  wananchi  wa wilaya   hiyo katika mazishi ya  kiongozi huyo.

Mbunge  Filikunjombe  alisema  kuwa  CCM wilaya ya  Ludewa  imempoteza  kiongozi mchapa  kazi na aliyekuwa na uwezo  mkubwa katika  kukitumikia  chama ngazi ya  wilaya na Taifa na  kuwa kati ya  vijana  ambao wamekuwa mbele  kujenga  chama katika  wilaya   hiyo ni pamoja na marehemu huyo kwani  siku  zote za  uhai  wake alikuwa  ni mhumini mzuri  wa kunadi  sera  za CCM na hakuwa kiongozi mwenye majivuno  wala makundi.

Hivyo  alisema  kuwa  kifo  cha MNEC  huyo kimekuja  huku  wilaya ya  Ludewa ikiwa katika maandalizi ya  kuanzimisha miaka 38  ya kuzaliwa kwa  CCM sherehe  iliyopangwa  kufanyika siku ya jumapili  ya February 8 mwaka   huu kwa mara ya kwanza katika kata ya Kilondo mwambao mwa ziwa nyasa  lakini kutokana na msiba  huo  mkubwa sherehe   hizo  zitasogezwa  mbele  hadi Februari  15 mwaka  huu.

" Mimi   pia nilikuwa  nikijiandaa  kwa ajili ya  kuanza  safari ya  kuelekea  wilayani Ludewa  katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa  kwa CCM kama mgeni  rasmi ila sitaweza  kufanya   hivyo na  chama  kimeamua  kusogeza  sherehe  hizo hadi jumapili ya ijayo  ili  kupisha maombolezo kwa  wana CCM kwa  kifo  cha kiongozi   huyo"

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI