AUA MKEWE NA KUMZIKA KWENYE ZIZI LA NG'OMBE

MWANAMKE  mmoja mkazi wa kata ya Ubetu Kahe wilaya  ya  Rombo mkoani
Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya  kuuawa na mumewe na kisha mwili
wake  kwenye boma la ng’ombe.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro  Geofrey Kamwela  amethibitisha
kuuawa kwa mwanamke huyo na kusema tukio hilo limetokea Februari 25
mwaka huu saa 11:45 jion katika nyumba waliyokua wakiishi.

Kamanda amemtaja  Mwanamke huyo kuwa ni  Jenipher Peter (45) na kuwa
kifo cha mwanamke huyo kinatokana na kipigo alichokipata kutoka kwa
mumewe.

Alisema mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina la Peter Mrosso (43)
mara baada ya  kumuua mkewe alimfukia kwenye boma la  kulishia mifugo
mifugo na kisha kumpigia simu jirani akijitapa kuwa  amemuua mkewe.

Akielezea  tukio hilo, kamanda  alisema siku ya  tukio jirani wa
familia hiyo alipigiwa simu na Mume wa Marehemu na kumweleza kuwa
amemuua mkewe na kumtelekeza ndani ya Boma la Ng’ombe.

Kamanda alisema taarifa za mauaji ya mwanamke huyo ilitolewa baada ya
Jirani yake kupigiwa simu na Mume wa Marehemu, akimtaarifu kuwa
amemuua mkewe na maiti ameifukia ndani ya Boma la Mifugo.

Alisema baada ya jirani huyo kupewa tarifa hizo, alikwenda kutoa
taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji aitwaye Aloyce Swai (51) na
walipofika eneo la tukio waliukuta mwili wa Marehemu umefukiwa na
udongo na kubakishwa sehemu ya kichwa ikiwa juu.

Baada ya mwili wa Marehemu huyo kufukuliwa ulikutwa ukiwa na majeraha
sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na  Puani na kwamba
baada ya mtuhumiwa kufanya unyama huo alitokomea kusiko julikana .

Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika, na kwamba
jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi pamoja na kumsaka mtuhumiwa,
ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU