Balozi
wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akisalimiana na Daktari bingwa wa
Afya ya jamii na familia, Dkt. Ali Mzige kwenye hafla fupi ya kukabidhi
madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo
yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo
hapa Tanzania, BANGO SANGHO. Katikati ni Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine
Ndungulile.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Balozi
wa India nchini, Mh. Debnath Shaw (wa pili kulia) akiteta jambo na
Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (kulia) kwenye hafla fupi
ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi
Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali
waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.
Balozi
wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akipokea zawadi ya maua kutoka kwa
mmoja watoto wa shule ya msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally (kushoto) akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Balozi wa India nchini
Tanzania, Mh. Debnath Shaw kuzungumza na wageni waalikwa.
Balozi
wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akizungumza na wazazi, walimu na
wanafunzi wa shule ya msingi Kibugumo kwenye hafla ya kukabidhi madawati
50 na majengo mawili yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka
India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.
Baadhi
ya wajumbe wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa
Tanzania, BANGO SANGHO wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.
Mbunge
wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi madawati 50 pamoja na majengo mawili yaliyokarabatiwa na umoja
wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO
SANGHO katika shule ya msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania,
BANGO SANGHO, Amit Nandy akielezea nia na madhumuni ya umoja huo ambao
utaendelea kusaidia jamii zenye uhitaji kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
ikiwa ni pamoja na kudumusha ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na
India.
Kaimu
Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Angelina Ngasazwa akitoa neno la
shukrani kwa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa
Tanzania, BANGO SANGHO kwa msaada walioutoa shule ya msingi Kibugumo.
Mbunge
wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akiongoza ugeni huo kuelekea eneo
la tukio kwa ajili ya zoezi la kukabidhi majengo mawili
yaliyokarabatiwa na umoja wa Bango Sangho.
Balozi
wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akikata utepe kuzindua moja ya
majengo ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii
ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO kwenye
hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kigamboni jijini Dar.
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine
Ndungulile (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu
kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy (wa
pili kushoto) Pintu Dutta na Dipankr ambao ni wajumbe wa umoja huo.
Balozi
wa India nchini, Mh. Debnath Shaw na Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dk.
Faustine Ndungulile wakikagua moja ya jengo la darasa lililokarabatiwa
na kuwekwa madawati mapya na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali
waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.
……………………………………..
Na Mwandishi wetu
WANAFUNZI
150 waliokuwa katika dhiki ya elimu shule ya msingi Kibugumo kutokana
na kulazimika kusoma wakiwa wameketi sakafuni wamekabidhiwa madawati
yatakayowawezesha kusoma kwa raha.
Madawati
hayo yamekabidhiwa jana na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali
waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO mbele ya shuhuda ya balozi wa India
nchini, Debnath shaw.
Pamoja na madawati hayo taasisi hiyo ilikabidhiwa madarasa mawili yaliyokarabatiwa.
Akipokea
msaada huo Kaimu Ofisa elimu wa Manispaa ya Temeke Angelina Nasazwa,
alisema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuangalia changamoto nyingi
zilizopo katika shule hiyo, ikiwemo miundombinu ya madarasa na ofisi.
Alisema
kukabidhiwa kwa madawati na majengo hayo kunapunguza shida iliyopo na
kufanya mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wengi kuwa rafiki.
Aidha
pamoja na kutoa shukrani kwa umoja wa Bango Sangho na pia kwa balozi
mwenyewe kwa kusaidia shule hiyo, ofisa huyo alisema kwamba jumuiya hizo
zimefanya vyema kuwakumbuka watoto hao ambao walikuwa na changamoto
kubwa za kusoma wakiwa wameketi huku wakiwa hawajui kwamba kwa matatizo
hayo wamekuwa wakikosa haki zao za msingi za elimu bora.
Hata
hivyo pamoja na kupokea misaada hiyo aliwataka watu Bango Sangho
kuendelea kutoa ushirikiano kwa shule hiyo ambayo inakabiliana na
changamoto nyingi.
Naye
Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile aliwapongeza watu wa Bango
Sangho kwa kuiona shule hiyo ya Kibugumo na kusema wananchi wa Kibugumo
watauenzi msaada huo kwa kutunza madawati na madarasa hayo ambayo
yamepatikana kutokana na kujinyima kwa wanachama wa Bango Sangho.
Pamoja
na kuomba ushirikiano pia mwalimu Tatu alisema upo uwezekano wa shule
hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 wakati wa kamepni za vijijini vya ujamaa,
kupata umeme kwa kuwa nguzo zimepita karibu kinachotakiwa kwa wahusika
kuliona hilo.
Naye
balozi wa India nchini amesema amefurahishwa kushuhudia uhusiano mzuri
uliopo kati ya wakazi wa Kibugumo na jamii ya India inayoishi nchini
Tanzania kupitia Bango Sangho.
Alisema
mchango wa wanajumuiya ya Bango Sangho ni muhimu hasa kipindi hiki cha
mabadiliko ya sera ya elimu itakayoanza kutumika mwakani, ambayo
inatarajia kuleta mapinduzi makubwa ya elimu nchini.
Mbunge
huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano na jumuiya hiyo huku akiahidi
ushirikiano pia katika uendesha kliniki kwa wanafunzi wa shule ya
Kibugumo.
Bango
Sangho ni jumuiya ya wananchi wa India wanaoishi nchini Tanzania ambao
hujishughulisha na masuala ya utamaduni na kidini na wakati mwingine
hutoka na kusaidia jumuiya zingine hasa watoto.
Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo Amit Nandy akimkaribisha mgeni rasmi balozi wa India
kuzungumza machache, alisema pamoja na majukumu ya jumuiya hiyo katika
masuala ya kidini na utamaduni,wamekuwa wakishirikiana na taasisi
nyingine kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
Alisema
walikabidhiwa jukumu la kusaidia shule hiyo miaka miwili iliyopita na
kwamba wanashukuru wametimiza azma hiyo na sasa wanataka kufanya
matibabu bure kwa wanafunzi kama kamati ya shule na serikali ya eneo
hilo itakubali.
Awali Mwalimu Tatu Mhina akisoma risala ya kuukaribisha ugeni huo
shuleni Kibugumo, alisema bado wana changamoto kubwa kubwa kutokana na
shule hiyo kuwa na wanafunzi 1000 huku wengi wao wakiwa na tatizo la
miundombinu, madarasa, ofisi za walimu na madawati.
Alisema pamoja na kwamba bado wana madarasa lakini madarasa yamechakaa na hivyo kuhitaji kuangaliwa.
Aidha
baadae mwalimu huyo katika mahojiano alisema kwamba wanachangamoto ya
chumba cha kompyuta na umeme na kwamba wanafundisha somo la tehema bila
uhalisia.
Comments