Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yatoa mafunzo kwa wataalamu wake


1Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akifungua mafunzo ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwa kutoa mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi mafunzo hayo yamefanyika kaktika ukumbi baraza la Maaskofu TEC jijini Dar es salaam.
..................................................................................
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi. Mafunzo hayo yalifunguliwa jana, na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Bw, Aziz Kilonge, ambaye aliwaasa wataalam hao kuhakikisha kwamba wanasimamia wanafunzi kwa ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti zinazofanywa. Aidha, alifafanua kuwa uzingatiaji wa maadili katika kufanya tafiti, ndio msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine. Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuandika ripoti na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. Hivyo lengo kuu ni kuwejengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa taifa. Aliwakumbusha wasimamizi hao kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kujiamini na kujieleza kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI