FAMILIA YA WATU SITA YATEKETEA KWA MOTO KIPUNGUNI DAR

 Majirani wakisaidia kukusanya baadhi ya mabaki baada ya nyumba ya Askari msitaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Mzee David Mpila iliyopo Kipunguni, Dar es Salaam kuteketea  kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme na kupoteza uhai wa maisha ya watu 6 wa familia moja akiwemo mzee Mpila.PICHA NA HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Waliofariki katika ajali hiyo ya moto iliyotokea alfajiri leo, ni Mzee David Mpila, Selina Mpila, wajukuu wawili Selina na Paulina, mtoto wa Mpina Lukas na shemeji wa Mpina.

Akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea, mmoja wa majirani wa nyumba hiyo, Richard Zakaria, alisema usiku saa 10, aliamshwa na mkewe na kumwambia watoke nje nyumba ya jirani inaungua moto.

Baada ya kutoka aliwakuta majirani wenzie wanne na kuanza kuhangaika kuzima lakini walishindwa kwani moto ulikuwa mkubwa mno, hivyo kuishia kutapatapa wasijue la kufanya.

Alisema kilichowasnagaza ni kutosikia sauti yoyote ya mtu kutoka ndani ya nyumba hiyo, kitendo ambacho kiliwafanya wafikirie kuwa huenda Mzee Mpila na familia yake wamenusurika kwa kutoka baada ya kuona nyumba inaungua.

Lakini mashaka yalizidi baada ya watu hao kutowaona nje hivyo kuingiwa na wasiswasi kwamba huenda wameungua ndani ya nyumba.

Zimamoto walifika majira ya saa 11, lakini hawakuweza kufanikiwa kuzima kwani nyumba ilikuwa imeteketea kabisa.

Saa 12 Miili ya marehemu ilichukuliwa na Polisi wa Kituo cha Staki Shari na kupelekwa Hospitali kuhifadhiwa.Mazishi yatafanyika Jumanne ijayo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi walioguswa na msiba huo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalumu, Profesa Mark Mwandosya aliyefika kuhani msiba huo, kwani yeye ni kaka wa mama mwenye nyumba aliyefariki

vIONGOZI WENGINE WALIOFIKA KWENYE MSIBA HUO, NI mKUU WA mKOA WA dCAR ES sALAAM, sAID sADIKI, MADIWANI NA VIONGOZI KADHAA WA SERIKALI.


 NDUGU WA KARIBU WAKILIA KWA UCHUNGU KWENYE MSIBA HUO
 Nyumba inavyoonekana baada ya kuteketea kwa moto


 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo
 majirani wakikusanya nguo na vitu vingine vilivyonusurika

 Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa (kulia0 akiwa miongoni mwa waombolezaji waliofika kwenye msiba huo
Mama akilia kwa uchungu katika msiba huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI