⌂ Home ๐Ÿ‘ค Richard ⚙ Help Press ? for keyboard shortcuts. 1 KAMPUNI YA TRUMARK YAANDAA WARSHA MAALUMU KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu warsha maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 7, 2015 ukumbi wa Mlimani City. Wengine kutoka kushoto ni maofisa wa Trumark,  Antu Mandoza na Nuru Lyau.
 Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza 
jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa warsha hiyo, Nuru Lyau.
 Ofisa wa Kampuni ya Trumark, Zulekha Samwix (kulia), akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
  Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza 
jambo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya TruMark ya jijini Dar es Salaam imeandaa warsha yenye lengo la kumjengea mwanamke uwezo wa kutambua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.

Hayo yamemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Agness Mgongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mgongo alisema warsha hiyo itafanyika Machi 7, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa  Mlimani City ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

'Tunataka tumjengee mwanamke uwezo wa kujiamini, kujithamini na kutambua kuwa changamoto anazozipata ni fursa zitakazomfanya aweze kupambana na makali ya maisha na kisha kujiendeleza bila kumtegemea mwanaume' alisema Mgongo.

Aidha Mgongo alisema kuwa warsha hiyo itajumuisha shuhuda na maonesho ya bidhaa na kazi za mikono kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kupitia changamoto mbalimbali walizozipitia.

'Siwezi kuwataja ila watakuwepo wanawake ambao walikumbwa na changamoto mbalimbali lakini hawakukata tamaa na mwisho wa siku wakafanikiwa,' alisema Mgongo.

Naye kwa upande wake Mratibu Mkuu wa warsha hiyo, Antu Mandoza alisema kuwa kutakuwa na kiingilio cha sh. 50,000 ambayo asilimia 10 ya fedha zitazopatikana zitaelekezwa katika kuwaandaa wasichana kujitambua mapema kabla ya kuingia katika soko la ajira.

'Tutaenda katika shule mbalimbali za wasichana kuwafundisha mbinu nbalimbali za kuwa wajasiriamali na kujiajiri punde wanapohitimu masomo yao' alisema Mandoza.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA