Korea wameamua hivi kuhusu ishu ya wapenzi kuwa na michepuko…

3929-000026
Wakati TZ tunaendesha kampeni ya “Baki njia kuu..michepuko sio dili…epuka UKIMWI” ili kuhimiza watu wajiepushe na mazingira yatakayosababisha kupata maradhi hayo, leo ndio nafahamu kwamba kumbe Korea Kusin walienda hatua nyingine mbele zaidi ya hii, wao walikuwa na Sheria ambayo ilikuwa mtu ukikamatwa yani kwa kesi ya kuchepuka ni kama kesi nyingine tu, unapelekwa Mahakamani na wengi wameshahukumiwa vifungo kabisa.
Ripoti inaonesha toka mwaka 2008 watu zaidi ya 5,500 wamehukumiwa kwa kesi za kuwa na uhusiano nje ya ndoa, jana historia imegeuka kwao, limekaa jopo la Majaji tisa, saba kati yao wamekubali kuwa Sheria hivyo iondolewe.
Jaji  Park Han-Chul alikuwa mmoja ya walioshiriki kwenye jopo hilo, amesema imefika wakati wa kubadili Sheria za masuala ya uhusiano wa kimapenzi kwa watu wao; “Hata kama ishu ya kutoka nje ya ndoa ni kinyume cha maadili ya kijamii, Serikali haipaswi kuingilia masuala ya maisha binafsi ya watu“– Park Han-Chul.
Sheria hiyo ilipitishwa mwaka 1953 ambapo hukumu ilikuwa kama ukikutwa na hatia ya kumsaliti penzi wako kifungo ilikuwa mpaka miaka miwili jela, kwa maamuzi yaliyofanyika jana Sheria hiyo imetenguliwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*