MSAMA ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA VITUO VITANO VYA YATIMA NA WATU WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, AKEMEA MAUAJI YA ALBINO.

 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akikabidhi msaada wa vyakula na sabuni kwa Sudi Said kwa ajili ya Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza Kijiweni, katika hafla ya kutoa msaada kama huo kwa vituo vitano jijini Dar es Salaam jana,ikiwa ni sehemu ya mapato aliyopata katika tamasha la mwaka jana. Tamasha hilo linalotimiza miaka 15 mwaka huu litafanyika jijini Dar es Salaam Aprili 5. (PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Msama ambaye ametoa vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 5, yupo katika harakati za maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam, litakaloshirikisha wasanii maarufu wa muziki wa injili wa ndani na nje ya nchi.Tamasha hilo linatimisha miaka 15 tangu lianzishwe mwaka 2000.

Pia, wakati wa makabidhiano hayo, Msama alikemea vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi unaoendelea nchini ambapo aliwaomba viongozi wa kimila, kidini na kisiasa kukemea kwa nguvu mauaji hayo.

Aidha, Msama aliishauri Serikali kuweka utaratibu wa kuokoa mauaji hayo kwa kuwakusanya watoto albino nchini kote na kuwajengea eneo ambalo wote wataishi hapo kwa kuwapatia ulinzi mkali hadi wakapokuwa watu wazima ndipo waruhusiwa kuondoka.
 Msama akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Honoratha cha Temeke, Honoratha Michael msaada wa vyakula hivyo


 Katibu wa Kituo cha Yatima cha Maunga Centre cha Kinondoni, Rashid Mpinda akipokea  msaada huo
 Khadija Mwambungu akipokea  msaada huo kutoka kwa Alex Msama kwa ajili ya kituo chake
 Mratibu wa Tamasha hilo Hudson Kamoga akielezea jinsi maandalizi ya tamasha hilo yalivyopamba moto
Msama akiwa amewabeba watoto wanaolelewa katika Kituo cha Honorathe Temeke, Gaston Edwin (kushoto) na Haid Edwin wote raia wa Marekani

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.