MTOTO CRISTNER ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KWA KUTESWA NA MAMAKE


Mtoto Cristiner Kusale (2) aliyedaiwa kuteswa na mama yake mzazi kwa kupigwa na  kuchomwa na kitu chenye incha kali kisha kufungiwa ndani, akiwa amelazwa kuendelea na  matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam juzi. (PICHA NA WITNESS ROBERT)

 NA MWANDISHI WETU

MTOTO aliyedaiwa kuteswa na mama yake mzazi kwa kupigwa na  kuchomwa na kitu cha incha kali kisha kufungiwa ndani, Cristiner Kusale (2) anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitalini ya Mwananyamala.

Akizungumza jana jijini Dar es Salam na Jambo leo hospitalini hapo Daktari wa watoto kutoka kitengo cha watoto afya na jamii,Innocent Michael alisema mtoto kristianer alipokelewa hospitalini hapo februari 23 mwaka huu.

Akiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na vidonda vingi vilivyonekana kama amechoma na kitu cha chenye ncha kali kilichowekwa motoni.

''Ilidaiwa kuwa huyu mtoto alikuwa anaishi na mama yake mzazi lakini hayaonekana hapa hospitalini na mtoto cristiner aliletwa hapa hospitalini kwa msaada wa majirani,''alisema.

Dk Michael alieleza kuwa mtoto huyo baada ya kufanyiwa vipimo alingulika kuwa anautapiamlo na pia kutokana na majeraha aliyokuwa nayo mwilini alikuwa katika hatari ya kupata kansa ya damu.

''Mtoto amebainika kuwa na utapiamlo na afya yake hairidhishi kama ya mtoto mwenye miaka miwili hivyo inaonekana alikuwa hapatiwi chakula cha rishe kwa wakati,''alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na matibabu anayoendelea kuyapata hospitalini hapo yamemsaidia cristianer kutokuwa katika hatari ya kupatwa na kansa ya damu.

Alieleza vidoda vinapokuwa wazi vinasababisha bateria wachafu kuingia ndani ya mwili kupitia majeraha na hinyo aliwashukuru wamajamii kwa kumfikisha mtoto huyo hospitalini hapo mapema.

Dk Michael alitumia muda huo kuitaka jamii kuwa na mshikamano wa kuwafikisha watoto kama hao hospitalini mapema ili kupatiwa matibabu na kuepuka na magojwa ya kuambukizwa.

"Naishukuru jamii na majirani waliokuwa karibu na mtoto huyu na kumfikisha hospitalini hapa kwapatiwa matibabu mapema,"alisema.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Camilius Wambura alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye ni mama mzazi na Cristiner anashikiliwa na polisi katika kituo cha Ostabay kinondoni.

mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI