PSPF WATOA SEMINA KWA ASKARI NA WATUMISHI RAIA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI JIJINI DAR

Afisa Matekelezo Mwandamizi(SCO) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Matilda A. Nyallu  akitoa elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam
 
Askari na watumishi raia wakifuatilia elimu hiyo iliyokuwa inatolewa na maafisa wa PSPF waliofika makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani kutoa elimu ya  Mpango wa Uchangiaji wa Hiari

Mfuko wa penseni wa PSPF ulipata fursa ya kukutana na kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali wanazo zitoa na kuweza kuwapa maelezo ya baadhi  ya mafao yanayo tolewa kupitia  Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa (PSS)  kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dae es Salaam.

Bi. Matilda A. Nyallu ambaye ni Afisa MatekelezoMwandamizi(SCO) wa mfuko wa PSPF  aliweza kutoa rai kwa Askari na watumishi raia wote waweze kujiunga na mfuko wa jamii wa PSPF ili kuweza kupata mafanikiona kunufaika , Pia alitoa mifano michache kwa ambao watajiunga .
 na mfuko huo ambapo kwa Askari na watumishi raia alitaja kuwa wanaweza kupata  mikopo ya kuanzia maisha ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wa nyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama.
Hata hivyo afisa wa mfuko wa Pensheni Bw.hadji Jamadary aliweza kuwaasa na kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga mfano kutoka kwao.
Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali .Hata hivyo afisa wa mfuko wa Pensheni Bw.hadji Jamadary aliweza kuwaasa na kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga mfano kutoka kwao.

Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI