RAIS KIKWETE AWATIMUA WAKUU WA WILAYA 27


RAIS Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 27 pamoja na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya wakuu wa wilaya wa mwanzo kwa lengo la kuboresha utendaji Serikalini.

Akitangaza wakuu hao wa wilaya mjini hapa jana ,Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa,mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi 27  zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Alizitaja sababu hizo kuwa ni kufariki kwa wakuu wa wilaya watatu,wakuu wa wilaya watano kupandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa ,wakuu wa wilaya saba kupangiwa majukumu mengine huku wakuu wilaya 12 wakitenguliwa uteuzi wao.

Alisema katika mchakato huo,wakuu wa wilaya 64 wamebailishwa vituo vya kazi na wakuu wa wilaya 42 wameendelea katika vituo vyao vya kazi vya awali.

Pinda aliwataja waliwataja wakuu wa wilaya wapya kuwa ni pamoja na Mariam Mtima (Ruangwa),Dk.Jasmine Tiisike (Mpwapwa),Pololeti Mgema (Nachingwea),Fadhili Nkurlu (Misenyi),Felix Lyaniva (Rorya),Fredrick Mwakalebela (Wanging'ombe) na Zainabu Mbussi (Rungwe) .

Francis Mwonga(Bahi),Kiming'ombe Nzoka (Kiteto),Husna Msangi (Handeni),Emmanuel Uhaula (Tandahimba),Mboni Mhita  (Mufindi),Hashim Mgandilwa (Ngorongoro) ,Mariam Juma (Lushoto),Thea Ntara (Kyela),Ahmad Nammohe (Mbozi) na Shaaban Kisu ( Kondoa).

Wengine ni  Zelothe Steven (Musoma),Pili Moshi (Kwimba),Mahmoud Kambona (Simanjiro) ,Glorius Luoga (Tarime),Zainabu Telack (Sengerema),Benard Nduta (Masasi),Zuhura Ally (Uyui) ,Paul Makonda (Kinondoni),Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na Maftah Mohamed (Serengeti).

Vile vile Pinda aliwataja waliotenguliwa uteuzi wao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo sababu za kiumri ,kiafya kuwa ni pamoja na James Millya aliyekuwa Mkuu we wilaya ya Longodo,Elias Lali aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Alfred Msovella aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa ,Danny Makanga aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kasulu,Fatma Kimario aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Wengine waliotenguliwa  ni Elibariki Kingu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Igunga,Dk.Leticia Warioba aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Iringa ,Evaristi Kalalu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi,Abiud Saidea aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Momba,Martha Umbulla aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kiteto,Khalid Mandia aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Babati na Elias Goroi.

Aidha Pinda aliwataja wakuu wa wilaya ambao uteuzi wao umetenguli na kupangiwa majukumu mengine ni wakuu wa wilaya saba ambao ni Brigedia Generali Cosmas Kayombo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Kanali Ngemela Elson Lubinga aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mlele na Juma Madaha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ludewa.

Pia  wamo,Mercy Silla aliyekuwa mkuu wa wilaya Mkuranga,Ahmed Kipozi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Mrisho Gambo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe na Elinas Pallangyo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Rombo.

Kwa  mujibu wa Pinda  wakuu wa wilaya waliofariki kuwa ni  Kaptein Yamungu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti,Anna Magoha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Urambo na Moshi Chang'a aliyekuwa mkuu  wa wilaya ya Kalambo.

Waziri Mkuu Pinda amewataka wakuu wa wilaya waliobadilishwa vituo kuanza kazi mara moja huku akisema wapya wanasubiri kupatiwa mafunzo ili kuboresha uwajibikaji wao.

xxxxxxxx

Joyce Kasiki,Dodoma

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema taarifa za Mfuko wa Pensheni wa PSPF zinaonesha limbikizo la mikopo ya serikali hadi kufikia desemba 2014 ni sh.bilioni 517.9 huku madeni ya mifuko yote ya hifadhi ya jamii kwa serikali ni shilingi trilioni 1.8.

Waziri Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo wakati akifungua   Mkutano wa Nne wa mwaka wa wadau wa Mfuko huo uliofanyika mjini hapa alisema ,malimbikizo ya michango ya watumishi wa Serikali hadi hadi ilipofanyika tathmini ya mfuko huo mwaka 2010 ni sh.Trilioni 4.04.

Pinda alisema,  madeni hayo yamekuwa yakiathiri shughuli za mifuko hususan  katika Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na mifuko hiyo.
 
"Lakini hata hivyo,Serikali imeandaa mkakati wa kuyashughulikia na kuondoa hofu kuhusu  taarifa zilizopo kwamba mifuko hiyo ipo katika hatari ya kufa kutokana na madeni hayo." alisema Pinda
 
Alisema , baadhi ya athari za madeni hayo kuwa ni pamoja na kupunguza uwezo wa mfuko kulipa wanachama kwa wakati,kushindwa kuwekeza kabisa kitu ambacho hakitatokea kwa sababu serikali, malalamiko kutoka kwa wastaafu kuhusu kucheleweshwa malipo yao.
 
"Serikali  imeshaanza kulipa sehemu ya deni hilo na taarifa za Hazina zinaonesha hadi sasa shilingi bilioni 160 zimelipwa kwa upande wa PSPF na anaelewa changamoto iliyopo ni kasi ndogo ya malipo."
 
 
Aidha alibainisha alisema malalamiko ya wanachama wa Mfuko huo ya kucheleweshewa malipo ya mafao yao yanaweza kupatiwa ufumbuzi na mfuko huo.

Alisema yapo malalamiko ya wanachama wengi wanaojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba upo usumbufu mkubwa katika kupata taarifa sahihi kutoka kwenye mfuko.

“Upo ucheleweshaji mkubwa katika malipo ya pensheni pale mfanyakazi au mwanachama anapostaafu , Vile vile lipo tatizo la wanachama kutoridhishwa na faida ya uwekezaji, Malalamiko haya yanaweza kabisa kupatiwa ufumbuzi,”alisema Pinda

Hata hivyo alisema takwimu zilizopo zinaonyesha ni asilimia 5.9 tu ya nguvu kazi ya Watanzania waliopo katika sekta rasmi ndio wanaopata huduma ya hifadhi ya jamii huku akisema, takwimu hizo ni kielelezo tosha cha kuonyesha changamoto inayoikabili sekta ya hifadhi ya jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, alisema changamoto  kubwa inayowakabili ni watumishi ambao wanaokaribia kustaafu kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu zinazohitajiika ili ziweze kusaidia katika kuandaa mafao yao kwa wakati.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi  ya wadhamini ya mfuko wa PSPF,George Yambesi aliiomba Serikali kuongeza kasi ya ulipaji wa deni la mfuko huo ili mfuko huo uweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
 
 
Waliobadilishwa vituo ni
Nyerembe Munasa anatoka Arumeru anakwenda Mbeya, Jordan Rugimbana alikuwa Kinondoni anakwenda Morogoro, Fatma Salum Ally kutoka Chamwino kwenda Mtwara, Lephy Gembe kutoka Dodoma Mjini kwenda Kilombero na Christopher Kangoye kutoka Mpwapwa kwenda Arusha.
Wengine ni Omar Kwaang’ kutoka Kondoa kwenda Karatu, Francis Mtinga kutoka Chemba kwenda Muleba, Elizabeth Mwasa kutoka Bahi kwenda Dodoma, Agnes Hokororo kutoka Ruangwa kwenda Namtumbo, Regina Chonjo kutoka Nachingwea kwenda Pangani, Husna Mwilima kutoka Mbogwe kwenda Arumeru na Gerald Guninita kutoka Kilolo kwenda Kasulu.
Wengine waliobadilishwa vituo vya kazi ni Zipora Pangani kutoka Bukoba kwenda Igunga, Kanali Issa Njiku kutoka Misenyi kwenda Melele, Richard Mbeho kutoka Biharamuro kwenda Momba, Lembris Kipuyo kutoka Muleba kwenda Rombo, Ramadhani Maneno kutoka Kigoma kwenda Chemba, Venance Mwamoto kutoka Kibondo kwenda Kaliua, Gishuli Charles kutoka Buhigwe kwenda Ikungi, Novatus Makunga kutoka Hai kwenda Moshi na Anatory Choya kutoka Mbulu kwenda Ludewa.
Wengine ni Christine Mndeme kutoka Hanang’ kwenda Ulanga, Jackson Musome kutoka Musoma kwenda Bukobna, John Henjewele kutoka Tarime kwenda Kilosa, Dk Norman Sigalla kutoka Mbeya kwenda Songea, Dk Michael Kadeghe kutoka Mbozi kwenda Mbulu, Cripin Meela kutoka Rungwe kwenda Babati na Magreth Malenga kutoka Kyela kwenda Nyasa.
Said Amanzi kutoka Morogoro kwenda Singida,Antony Mtaka kutoka Mvomero kwenda Hai, Elias Tarimo kutoka Kilosa kwenda Biharamulo, Francis Miti kutoka Ulanga kwenda Hanang’,  Hassan Masala kutoka Kilombero kwenda Kibondo, Angelina Mabula kutoka Butiama kwenda Iringa, Farida Mgomi Kutoka Masasi kwenda Chamwino, Wilman Ndile kutoka Mtwara kwenda Kalambo.
Ponsian Nyami kutoka Tandahimba kwenda Bariadi,Mariam Lugaila kutoka Misungwi kwenda Mbogwe, Mary Onesmo kutoka Ukerewe kwenda Buhigwe, Karen Yunus kutoka Sengerema kwenda Magu, Josephine Matiro kutoka Makete kwenda Shinyanga, Joseph Mkirikiti kutoka Songea kwenda Ukerewe, Abdula Lutavi kutoka Namtumbo kwenda Tanga, Ernest Kahindi kutoka Nyasa kwenda Longido, Anna Nyamubi kutoka Shinyanga kwenda Butiama na Rosemary Kirigini kutoka Meatu kwenda Maswa.
Abdalla Ali Kihato kutoka Maswa kwenda Mkuranga, Erasto Sima kutoka Bariadi kwenda Meatu, Queen Mulozi kutoka Singida kwenda Ulambo, Yahaya Nawanda kutoka Iramba kwenda Lindi, Manju Msambya kutoka Ikungi kwenda Ilemela, Saveli Maketta kutoka Kaliua kwenda Kigoma, Bituni Msangi kutoka Nzega kwenda Kongwa na Lucy Mayenga kutoka Uyui kwenda Iramba.
Majid Mwanga kutoka Lushoto kwenda Bagamoyo, Muhingo Rweyemamu kutoka Handeni kwenda Makete, Hafsa Mtasiwa kutoka Pangani kwenda Korogwe, Dk Nassor Ali Hamid kutoka Lindi kwenda Mafia, Festo Kiswaga kutoka Nanyumbu kwenda Mvomero, Sauda Mtondoo kutoka Mafia kwenda Nanyumbu, Seleman Mzee kutoka Kwimba kwenda Kilolo, Ertirina Kilasi kutoka Wanging’ombe kwenda Muheza, Subira Mgalu kutoka Muheza kwenda Karagwe na Jacqueline Liana kutoka Magu kwenda Nzega.
Wanaobaki katika vituo vyao vya kazi
Wakuu wa wilaya wanaobaki katika vituo vyao ni Jowika Kasunga (Monduli), Raymond Mushi (Ilala), Sophia Mjema (Temeke), Amani Mwenegoha (Bukombe), Ibrahimu Marwa (Nywang’wale), Rodrick Mpogolo (Chato) Manzie Mangochie (Geita), Darry Rwegasira (Karagwe), Luteni Kanali Bnedict Kitenga (Kyerwa) na Constatine Kanyasu (Ngara).
Wengine ni Paza Mwamulima (Mpanda), Peter Kiroya (Kakonko), Hadija Nyembo (Uvinza), Dk Charles Mlingwa (Siha), Shaibu Ndemanga (Mwanga), Herman Kapufi (Same), Ephraimu Mbaga (Liwale), Abdallah Ulega (Kilwa), Joshua Mirumbe (Bunda), Deodatus Kinawiro (Chunya), Rosemary Senyamule (Ileje) na Galamhusein Shaban (Mbarali).
Wengine waliobaki ni Christopher Mgala (Newala), Barika Konisaga (Nyamagana), Sara Dumba (Njombe), Hanifa Karamagi (Gairo), Halima Kihemba (Kibaha), Nurdin Babu (Rufiji), Methew Sedoyeka (Sumbawanga), Idd Kimanta (Nkasi), Chande Nalicho (Tunduru)), Senyi Ngaga (Mbinga), Wilson Nkambaku (Kishapu) na Benson Mpesya (Kahama).
Wengine ni Paul Mzindakaya (Busega), Georgina Bundala (Itilima), Fatma Toufiq (Manyoni), Luten Edward Ole Lenga (Mkalama), Hanifa Selengu (Sikonge), Seleman Kumchaya (Tabora), Mboni Mgaza (Mkinga na Seleman Liwowa (Kilindi).
Waliopandishwa cheo ni John Mongela aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arusha amekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Amina MAsenza aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela amekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa,Dk.Ibrahim Khamis aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Moshi amekuwa mkuu wa mkoa wa katavi ,Halima  Dendego aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Tanga amekuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara na Daud Ntibenda aliyekuwa mkuu wa wilaya amekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.