TAMASHA LA PASAKA LASOMESHA YATIMA 350, YATOA MITAJI KWA WAJANE YENYE THAMANI YA SH. MIL 79

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, ambapo alielezea ujio wa wasanii wa muziki wa injili kutoka nchi za Afrika Kusini, Zambia,Malawi, Rwanda, Kenya na Burundi.

Pia alielezea jinsi tamasha hilo lilivyosaidia kusomesha watoto yatima 350 na kutoa misaada mbalimbali ya vyakula na vifaa kwa vituo vya kulelea wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo wajane wamepatiwa mitaji yenye yenye thamani ya sh. mil. 79.

  Amesema kuwa kuwa kwa vile Tamasha la Pasaka lipo kwa watu wasiojiweza, kamati imeamua kujenga Kituo Kikubwa  nchini cha kutolea misaada mbalimbali kwa ajili ya watu hao

Pia alikemea mauaji ya Albino yanayoendelea nchini, ambapo ameishauri serikali kkuwakusanya watoto alibino na kuwaweka sehemu moja ambayo watapata huduma ya ulinzi na malazi hadi watakapokuwa ndipo waruhusiwe kutoka katika kambi hiyo.

Pia aliwaasa viongozi wa siasa kuacha tabia za kishirikina ya kushawishika kutumia vioungo vya albino kwa lengo la kupata vyeo.

.Tamasha hilo linatarajia kufanyika Aprili 5,mwaka huu. Kushoto ni mmoja wa Wajumbe wa kamati hiyo, Khamis Pembe. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.