TANZANIA NA MAREKANI WASHEREHEKEA USAMBAZAJI WA VITABU MILIONI 2.5 KWA AJILI YA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI
Wananchi waliojitokeza katika sherehe
ya makabidhiano ya vitabu milioni 2.5 vya sayansi na hisabati kwa shule
za sekondari za serikali nchini. Vitabu hivyo kutoka serikali ya watu
wa Marekani vilikabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Marekani
nchini, Mark Childress katika hafla iliyofanyika Shule ya Sekondari
Mtakuja Beach iliyopo Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam leo. Hafla
hiyo ilifanyika katika shule hiyo kwa niaba ya shule zote za serikali
nchini.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa
Marekani nchini, Mark Childress wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja Beach huku wakiwa wameshika
baadhi ya vitabu walivyokabidhiwa katika sherehe hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi vitabu hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akihutubia
kwenye hafla hiyo.
Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni ambayo ilikuwa mwenyeji wa sherehe hizo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Marekani nchini, Mark
Childress (kushoto), akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete sehemu ya vitabu
ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya vitabu milioni 2.5 vya sayansi na
hisabati vilivyotolewa na serikali ya Marekani kwa ajili ya shule za
sekondari za serikali nchini katika hafla iliyofanyika Shule ya
Sekondari Mtakuja Beach iliyopo Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam leo.
Hafla hiyo ilifanyika katika shule hiyo kwa niaba ya shule zote za
serikali nchini. Vitabu hivyo tayari vimesambazwa katika shule hizo
nchini.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja Beach wakishangilia katika sherehe hiyo.
Wanawake wakicheza wimbo wa Christian Bela wa Mama.
Wadau wa elimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanawake wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete
akiwasili kwenye sherehe hizo.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda akiteta jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk.Shukuru Kawambwa wakati wakimsubiri Rais Kikwete awasili.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf
Mwenda (kulia), akitoa taarifa ya shughuli za maendeleo katika sekta ya
elimu mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakitoa burudani katika hafla hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Comments