TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KITUO CHA AFYA MBAGALA

 Mratibu wa Takwimu wa Manispaa ya Temeke, aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk. Samuel Lema (wa pili kulia) akimshukuru Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Alen Mwebuga (kushoto), baada ya kukabidhiwa jana kisima kipya kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil 24 katika Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table Dar es Salaama. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Batuli Luhanda.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table,Dk. Batuli Luhanda akimshukuru Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Alen Mwebuga (kushoto), baada ya kituo hicho kukabidhiwa jana kisima kipya kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil 24.Kulia kwake ni Mratibu wa Takwimu wa Manispaa ya Temeke, aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk. Samuel Lema.
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya kampuni hiyo ya kuboresha sekta ya maji katika baadhi ya hospitali, Vituo vya Afya na zahanati nchini, Kulia ni Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Alen Mwebuga
 Mratibu wa Takwimu wa Manispaa ya Temeke, aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk. Samuel Lema akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo wa kisima na kuahidi kukitunza.
 Makati wa Afya wa kituo hicho,Ruth Temba (kushoto)na  Samira Kondo  wakishiriki katika hafla hiyo
 Mama mkazi wa Mbagala, Khadija Ali akitoa shukrani kwa TBL  kwa msaada huo wa kisima ambapo alisema kisaidia sana kupunguza tatizo la maji lililokuwa linakikabili kituo hicho kinachozalisha wajawazito 20 kwa siku.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*