BAADA YA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KAPTENI KOMBA,KINANA AANZA ZIARA MKOANI DODODMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo asubuhi akitokea Mkoa wa Ruvuma ambako yeye na viongozi wengine walishiriki mazishi ya aliyekuwa Kiongozi wa Kikundi cha CCM cha uhamasishaji cha Tanzania One Theatre (TOT), Marehemu Kapteni John Komba.

Komredi Kinana pamoja na Katibu na Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye, wameanza ziara ya siku tisa Mkoa wa Dodoma, iliyokatishwa baada ya kutokea msiba wa Kapteni Komba, ili kutoa ushiriki katika msiba huo mkubwa ndani ya chama hicho.

Leo ziara imeanza katika Wilaya ya Mpwapwa, ambapo atakagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.




Komredi Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa baada ya kuwasili Dodoma leo.
Katibu wa  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mwanaamani Mtoo, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana.
Nape akizungumza mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Mpwapwa. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Komredi Kinana kushoto.

Nape akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA