LEO
katika maswali matano kuelekea miaka 15 ya Tamasha la Pasaka
linalotarajia kufanyika baadaye mwaka huu hapa Tanzania, Mbunge wa
Kuteuliwa, James Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
NCCR-Mageuzi ni shabiki mkubwa wa tamasha hilo lililoasisiwa tangu mwaka
2000 ambaye anakiri aliwahi kuhudhuria baadhi ya matamasha hayo na
kujionea waimbaji wa Tanzania wanavyofikisha ujumbe wa neno la Mungu
kupitia uimbaji.
Swali: unaizungumziaje sikukuu hii kubwa kuliko zote kwa Wakristo hapa duniani, ukiwa ni muamini wa dini hiyo?
Jibu: Nawaomba
Watanzania kujiandaa kusherehekea Sikukuu hiyo ambayo ni kubwa zaidi ya
zote duniani kwani tunasherehekea kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo
aliyefufuka kwa ajili ya kuwakomboa waumini mbalimbali ulimwenguni.
Swali: Nini wito wako kwa waumini katika sikukuu hiyo muhimu zaidi?
Jibu: Wito wangu kwa waumini kwanza ni kutambua maana ya Pasaka na kwanini tunasherehekea sikukuu hiyo adhimu hapa duniani.
Pili
nawaomba Watanzania wenzangu kujua maana ya Pasaka kwani hata Wakristo
baadhi hawatambui maana ya Pasaka na kwanini tunasherehekea sikukuu hii
muhimu ya kukumbuka ufufuko wa kipenzi chetu.
Swali:Nini wito wako kwa Tamasha la Pasaka ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions?
Jibu: wito
wangu kupitia Tamasha la Pasaka ambalo ni ufufuko wa Bwana Yesu
Kristo, Watanzania tulitumie kutenda mema yanayomfurahisha na kumpendeza
Mungu, kwani sasa hivi kuna matukio mengi machafu yanayomuudhi na
kumchukiza Mungu, hivyo ni nafasi yetu kumpigia magoti na kumuomba.
Kwani
tamasha hilo la muziki wa Injili si la Wakristo pekee, linashirikisha
mashabiki mbalimbali wa muziki huo wenye mwelekeo wa kuzungumza na Mungu
kupitia Waimbaji wanaopanda jukwaani ambao wanapaza sauti zao
zinazokwenda mbali zaidi kwa lengo la kumpigia magoti na kumuomba Mungu.
Swali: Unawaasa
nini Watanzania kupitia tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kusaidia
jamii zenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na wenye shida
zinazofanana na hizo ambazo zinahitaji msaada kutoka kwa wenye huruma
kama Alex Msama?
Jibu: Wito
wangu kwa Watanzania ni kuongeza upendo ili kuilinda amani yetu
tuliyonayo tuliyoachiwa na muasisi wa taifa hili, marehemu Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere ambaye alituasa tupendane kwani hata maandiko
matakatifu yanatueleza juu ya upendo baina ya wanadamu.
Amani
na upendo linatakiwa lizingatiwe kwa sababu, tunashirikiana na nchi
jirani kupitia waimbaji na hata viongozi kadhaa ambao wanashiriki kwenye
tamasha hilo ambalo linakusanya nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Afrika
Kusini, Zambia, Kenya, Rwanda na moja ya bara la Ulaya ambayo ni
Uingereza, jambo ambalo ni la kujivunia zaidi kwa sababu inaonesha sala
zetu zinafika kwa Mungu ipasavyo kwani kadri siku zinavyozidi kwenda
mbele idadi ya wageni kupitisa tamasha hilo wanazidi kuongezeka, hivyo
ni nafasi yetu kuitunza na kuithamini tunu hiyo muhimu tuliyopewa na
Mungu.
Kanuni
ya utu, binaadamu wote ni ndugu moja, mambo ya kuuana wenyewe kwa
wenyewe, uhasama, ufisadi, mauaji ya albino na machafu mengine
yanayochafua taswira na uongozi wa mataifa mbalimbali hasa Tanzania
iliyogubikwa na wingu hilo zito yatapungua kupitia Tamasha la Pasaka
ambalo ndio nguzo kuu ya kuondoa udhaifu huo.
Swali:
Nini changamoto iliyoko mbele hasa kwa masuala kama upitishwaji wa
Katiba pendekezwa, uchaguzi Mkuu na mengineyo yanayoendelea kabla ya
maendeleo hayo?
Jibu:Tamasha
la Pasaka mwaka huu lina changamoto nyingi kwani inatakiwa tujitafakari
kwa kiasi kikubwa tulipofikia na tunakokwenda kwani tunatakiwa turudi
katika umoja wetu tulioachiwa na baba wa Taifa Mwalim,u Julius Kambarage
Nyerere kwani Tanzania si wakabila bali ni Taifa moja, hivyo tuachane
na mifumo ambayo itaondosha umoja wetu na kutugombanisha kwa
kuchonganishwa na watu wachache wasioitakia mema nchi yetu.
Uchaguzi
mkuu wa mwaka huu una changamoto nyingi sana ambazo zisisababishe
tutoke kwenye mstari wa amani na upendo tulioachiwa na waasisi wetu kwa
sababu ya wachache wenye uchu wa madaraka ambao watatusababishia
machafuko ambayo yataigharimu nchi yetu.
Wito
wake kwa waimbaji wa Tanzania ni kuongeza juhudi ili kulinda na
kufanikisha maendeleo ya muziki huo ambao lengo lake ni kumfikishia
Mungu kilio chetu wanadam hasa kwa matukio yanayomchukiza.
Comments