JESHI LA POLISI MBEYA LAKAMATA WAPIGA RAMLI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangiakionyesha baadhi ya tunguli zilizokamatwa na jeshi lake.









     

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata watu 15 na kuwafikisha Mahakamani wakituhumiwa kujihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ikiwa ni hatua ya kuwasaka waganga wasiokuwa na vibari katika kukomesha maovu yanayotokana na imani za kishirikina.



Hayo yalithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  ambapo alisema kesi hizo zipo kwenye hatua mbali mbali.



Alisema kuwa katika msako ambao ulianza tangu Machi 6, mwaka huu, Tayari Jeshi hilo limewakamata waganga wa jadi 23 wanaojihusisha na upigaji waramli hizo chonganishi.



Msangi alisema  watuhumiwa 15 walifikishwa mahakamani na  kesi zao zipo katika hatua tofauti  na kwamba watuhumiwa sita  upelelezi bado unaendelea na mtuhumiwa mmoja taratibu zinafanywa ili aweze kufikishwa mahakamani.

Alisema  watuhumiwa walikamatwa katika wilaya tofauti na idadi yao kwenye mabano ambazi ni Wilaya ya Mbeya (7), Chunya(12) , momba(2),Mbozi (01) pamoja na Kyela(01).

Aidha Msangi alisema   baadhi ya zana ambazo wamekamatwa nazo waganga hao ni  pamoja na nyara vza serikali na zana zisizokuwa na nyara zisizokuwa za serikali .

Hata hivyo Kamanda Msangi alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na tabia za kusadiki  imani za ushirikina kwa kupiga ramli ili kutatua matatizo yao kwenye jamii.

Pia alitoa onyo kwa wananchi wanaoshirikiana  kuwaficha waganga wa kienyeji wanaojihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ambazo zinadaiwa kuwa chanzo cha uhalifu unaohusiana na imani za kishirikina.

Mwisho.
Picha na Mbeya yetu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU