KINANA AANZA RASMI ZIARA MKOA WA DODOMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto), akipita kwenye korongo kwenda kushiriki kupalilia shamba la Mkulima Bora wa Karanga, Anna Mlewa katika Kijiji cha Berege, wakati wa ziara yake wJimbo la Mpwapwa, mkoani Dodoma leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la karanga la mkulima bora Anna Mlewa katika Kijiji cha Berege, Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi

.Komredi Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, wameanza ziara ya siku tisa Mkoa wa Dodoma, iliyokatishwa baada ya kutokea msiba wa Kapteni Komba, ili kutoa ushiriki katika msiba huo mkubwa ndani ya chama hicho.

Leo ziara imeanza katika Wilaya ya Mpwapwa, ambapo atakagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Wananchi wa Kijiji cha Berege wakimlaki Kinana aliwapowasili kuzungumza nao


 Ni mapokezi ya aina yake katika Kijiji cha Berege

 Komredi Kinana akiondoka baada ya kukagua Kilimo la Umwagiliaji Katika Kijiji cha Msagali, Kata ya Chunyu


 Wananchi wa Kijiji cha  Msokwe, Jimbo la Mpwapwa, wakishangilia baada ya kumuona Komredi Kinana alipowasili kushiriki ujenzi wa Zahanati
 Kinana akisaidiana na Diwani wa Kata ya Mazae William Madaya kujenga zahanati ya Kijiji hicho Kisokwe.
 Komredi nKinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa hosteli iliyoungua katika Shule ya Sekondari ya Mpwawa.
 Kinana akiakgua jengo la hosteli ya Shule ya Sekondari ya Mpwapwa iliyoungua Januari 20, mwaka huu.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mpwapwa

 Mwalimu mstaafu Sylvester Oseah, akikishauri chama cha Mapinduzi (CCM), KUACHA KUWATEUA VIONGOZI WANAOTOA AHADI ZA UONGO KWA WANANCHI
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mpwapwa leo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*