KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Mathayo David Mathayo wakinywa maji ya bomba baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Gonjanza, Kata ya Suji, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Mathayo David Mathayo wakishiriki kufukia bomba la mji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Gonjanza, Kata ya Suji.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Mathayo David Mathayo alipowasili katika Shule ya Sekondari ya Njoro katika Jimbo la Same Magharibi ambapo alishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa.
 wananchi wakiwa wamejipanga kumlaki Komredi Kinana katika Shule ya Sekondari ya Njoro, Jimbo la Same Magharibi, mkoani Kilimanjaro leo.
 Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Mathayo David Mathayo akielezea mbele ya Komredi Kinana pamoja na wananchi jinsi miradi ya maendeleo ilivyotekelezwa katika jimbo hilo.
 Komredi Kinana akihutubia wananchi alipowasili katika Shule mpya ya Sekondari ya Njoro, katika Jimbo la Same Magharibi.
 Komredi Kinana akipatiwa zawadi ya silaha ya jadi pamoja na kuvishwa mgolole ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa  mmoja wa machifu wa kabila la Wapare. Tukio hilo lilifanyika katika shule ya Sekondari ya Njoro.
 Komredi Kinana akilakiwa na wananchi alipowasili katika Kijiji cha Makanya, Jimbo la Same Magharibi.
 Komredi Kinana akihutubia aliposimama kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Makanya, Jimbo la Same Magharibi
 Msafara wa Komredi Kinana ukielekea katika Kijiji cha Gonjanza, Kata ya Suji ambako alizindua mradi wa maji/

 Komredi Kinana akiwa na Nape baada ya kuwahutubia wananchi katika Kijiji cha Gonjanza, Kata ya Suji.
 Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria mkutano uliohutubiwa na Komredi Kinana katika Kijiji cha Gonjanza, Kata ya Suji.
 David Mathayo akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Gonjanza, baada ya Komredi Kinana kuzindua mradi wa maji.
 Komredi Kinana akihutubia wananchi katika Kata ya Hedaru, Jimbo la Same Magharibi
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Tawi la CCM Hedaru

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA