KOMREDI KINANA AKIWA KATIKA ZIARA JIMBO LA KIBAKWE LA SIMBACHAWENE

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua shamba la mfano la mahindi katika Mradi wa Wanyama Kazi, katika Kijiji cha Kibakwe wakati wa ziara yake katika Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma leo. Kinana yupo mkoani Dodoma kwa ziara ya siku tisa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.



 Msafara wa magari wa Komredi Kinana ukielekea Jimbo la Kibakwe kutoka Mpwapwa mjini, kuendelea na ziara yakuimarisha uhai wa chama
 Komredi Kinana akishiriki kupiga lipu chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari ya Ikuyu, Jimbbo la Kibakwe Mpwapwa.
 Komredi KIinana akishiriki kujenga Marumaru katika jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya Rudi, Jim,bo la Kibakwe.
Wananchi wakishangilia wakati Komredi Kinana alipokwenda kuweka Jiwe la Msingi la Ofisi ya Kata ya ya Mtamba, Jimbo la Kibakwe.
 Kinana akizungumza na wananchi huku akiwa na Mwenyekiti wa CCM TAWI LA Mtamba, jimboni Kibakwe, ambaye aliwezesha Kijiji cha Mtamba kuwa na wanaCCM asilimia 100
 Kinana akiondoka baada ya kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM Tawi la Mtamba
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Jimbo la Kibakwe, wilayani Mpwapwa.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adamu Kimbisa akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kibakwe, kabla ya kumkaribisha Komredi Kinana.
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kibakwe, ambapo aliagiza Halmashauri kuweka utaratibu mzuri wa kuwatengea vijana eneo katika machimbo  dhahabu ya madini ya Winza, badala ya kuwapatia wawekezaji wakubwa tu.
 Kinana akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Nyaulingo Bulamlete aliyekuwa akielezea kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa kisima cha maji mjini Kibakwe, ambapo alisema imebakia asilimia 10 tu kukamilika.
Mmoja wa wazee wa Mjini Kibakwe, akisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Stendi ya Kibakwe.
Kinana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Kapteni Chiku Galawa wakishiriki kupanda minyaa kwa ajili ya kuweka uzio wa mradi huo wa Wanyama Kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA