KOMREDI KINANA AMALIZA ZIARA MKOA WA DODOMA, ATUMIA KM 2289 KUKAGUA MIRADI 73 NA KUFANYA MIKUTANO 91

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Changaa, wilayani Kondoa, wakati wa ziara ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.


Katika ziara yake hiyo aliyoambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ilikuwa ya mafanikio makubwa, kwani msafara wake umetembelelea Wilaya 7 na majimbo mawili ya uchaguzi kwa kuzunguka jumla ya Km, 2289.

Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo mjini Kondoa, Nape alisema kuwa katika mkoa huo tayari wamefanya mikutano 91, ambapo 82 ya hadhara na 9 ya ndani. Pia wamekagua jumla ya miradi 73 ikiwemo 62 ya maendeleo na 11 ya chama.

Kesho Komredi Kinana na Nape Nnauye wanaanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha, ambapo wataanzia Jimbo la Monduli linaloongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.
 Wananchi wakinyoosha juu mikono kukikubali Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipoambiwa na Komredi Kinana KWAMBA WANAOKIKUBALI WANYOOSHE MIKONO JUU.
 Wananchi wa Kata ya Kwadelo wakinyoonsha mikono juu kukikubali Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko vyama vingine vya siasa. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni mstaafu Chiku Galawa akifafanua jambo wakati wa mkutano wa ndani, ambapo alisema ili kuondoa kabisa migogoro ya ardhi iliyopo katika ya Wakulima na Wafugaji tayari Serikali imeunda tume inayoshirikisha pia wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Morogoro, Manyara na Tanga. Kikao cha wakuu wa mikoa hiyo minne wamekutana usiku huu mjini Kondoa,
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa.

 Komredi Kinana akiondoka katika Kijiji cha Changaa baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho.
 Mkuu mpya wa Wilaya ya Kondoa, Shaban Kisu akijitambulisha wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Kisu ambaye alikuwa mtangazaji wa TBC ameteuliwa hivi karibuni na Rais kushika wadhifa huo.
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa Zabein Mhita akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Changaa.
 Komredi Kinana aakihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, ambapo amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukka pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
 Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi wakionesha vitu muhimu vilivyounguzwa na askari wa wanyamapori
 Wananchi wa Kijiji cha Kwadelo, wakimpatia zawadi ya silaha za jadi Komredi Kinana baada ya kufanya mkutano katika kijiji hicho.
 Komredi Kinana akiagana na wananchi wa Kijiji cha Pahi baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kilimo
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Komredi Kinana alipofanya mkutano katika Kijiji cha Kolo, wilayani Kondoa
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Zabein Mhita akijiandaa kupiga magoti ikiwa ni ishara ya kumuomba Komredi Kinana kusaidia kutatua tatizo la maji katika Mji wa Kondoa
 Nape Nauye akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi kuwa baadhi ya  vyama vya upinzani nchini viko hoi bin taabani
 Komredi Kinana akihutubia katika kmkutano wa kuhitimisha ziara ya siku tisa mkoani Dodoma leo.
 Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na nKatibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana.
 Nape akiungana kucheza muziki wa kikundi cha Talent Arts Group wakati wa mkutano huo

Kikundi cha sanaa cha Chemchem kikitumbuiza wakati wa mkutano huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU