KOMREDI KINANA ATINGA JIMBO LA MREMA MOSHI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji wa Himo, Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, amewaasa wananchi kuacha kujiunga na vyama vya upinzani ambavyo havina uwezo wa kuwasaidia kutatua kero zao, bali wajiunge na CCM yenye uwezo wa kutatua kero zao kwani ndo chama kinachoongoza serikali. Pia Kinana ameseam kuwa Umoja wa Vyama hivyo wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika uchaguzi ujao utageuka kuwa UKIWA akidai CCM itashinda  kwa Kishindo.
Komredi Kinana akisalimiana na Kamanda wa Vijana wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini alipowasili Kahe Magharibi kushiriki ufyatuaji katika kikundi cha vijana.Kikundi hicho kimewezeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kwa kupatiwa mashine 4 za kufyatulia matofali pamoja na sh. 500000 za mtaji.
Komredi Kinana akishiriki kufyatua matofali katika kikundi hicho cha vijana

Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana katika Kijiji cha  Kiruo Vunjo Kusini kata ya Uchira.
Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana katika Kata ya Uchira, Jimbo la Vunjo.
Komredi Kinana akihutubia wananchi katika Kata ya Uchira, Vunjo.
Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Jimbo la Vunjo, wakiwa katika mkutano na Komredi Kinana.
Wasanii wakitumbuiza wakati wa mkutano huo

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji wa Himo, Jimbo la Vunho, Moshi Vijijini.
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji wa Himo, Jimbo la Vunjo,Moshi Vijijini. Jimbo hilo linaongozwa na Mbunge wa TLP, Augustino Mrema.
Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa katika mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA