Napenda
Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye
Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya
leo,ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri
wangu,kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.pia
nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa
ndugu zangu woote (wakiwemo wazazi wangu wawili,Ankal Issa Michuzi,Ahmad
Michuzi,Karim Michuzi,Ramadhan Michuzi,Ismail Michuzi,Ankal Macheka,Ai
Michuzi,Zahra,Tatu,Sellah,Bobby,Noreen,Adam,Saleh na wengine wengi ambao
sijawataja majina yenu hapa ila moyoni ninayo,na bila kumsahau
mtarajiwa wangu wa ubani bi. Farida) kwa kuwa pamoja nami katika makuzi
yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.
Tanzania
Bloggers Network (TBN) pia naomba mpokee shukrani zangu za dhati kwa
kuwa pamoja nami kama mwanachama hai siku zote na bila kunitupa,pia
nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa TBN na wanachama
wenzangu kwa kuungana pamoja katika tafrija ya kihistoria
iliyotukutanisha pamoja,kiukweli ile ilikuwa ni siku muhimu sana kwetu
kwa kutukutanisha pamoja na kufahamiana zaidi,ile ilikuwa ni bonge la
heko kwani kuna wengine walitamani kuwa na umoja kama wetu lakini
hawafanikiwi.
pia nawashukuru marafiki,jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke.Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote. Nawapenda sana wote na tuko pamoja sana.TEMBELEA BLOG YA MTAA KWA MTAA Inayomilikiwa na Besdei boy Othman Michuzi kwa kufuata link hii. http://othmanmichuzi.blogspot.com
Hapa ni dole tupi,nikiwa na wadau wangu Anganile na Hellen Kiwia.
WAZIRI mKUU aendelea na ZIARA MBOZI mkoa wa mbeaya
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi na madaktari ya hospitali
ya mkoa wa Mbeya wakati alipofika hospitalini hapo kuwaona majeruhi wa
ajali ya askari wa kutuliza ghasia iliyotokea Februari 28, 2015 kati ya
Mbeyana Chuna.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji WP Cecilia Mussa mmoja wa askari
waliojeruhiwa akatika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha
Chang’ombe katika barabara ya barabara ya Mbeya Chunya Machi 1, 2015.
Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya na hali zao ni
nzuri.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimfariji WP Mwazanije Hassan mmoja
wa askari waliojeruhiwa akatika ajali ya gari iliyotokeakwenye kijiji
cha Chang’ombe katika barabara ya Mbeya Chunya Machi 1, 2015. Majeruhi
hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya na hali zao ni nzuri.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi wa Vwawa , Mbozi akiwa katika ziara ya mkoa wa mbeaya Machi 1, 2015
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakitazama ngoma ya kabila la
Wanyiha wakati walipotembelea kiwanda cha kusindika kahawa cha CMS
kilichopo Mbozi wakiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza maelezo kuhusu utafiti wa zao la kahawa
kutoka kwa Mtafiti Charles Mwingira wakati alipotembelea kituo cha
utafiti wa kahawa cha Mbimba , Mbozi machi 1, 2015.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua shamba la mfano la kahawa fupi wakati
alipotembelea kituo cha utafiti wa zao la kahawa akiwa katika ziara ya
mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akifungua maabara ya Shule ya Sekondari ya Vwawa akiwa kayioka ziara ya
mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro.
Comments