MAONESHO YA UTALII YA ITB YAANZA RASMI UJERUMANI

      

men1Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh. Philip Marmo katika picha ya pamoja na mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi za jumuia ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani sambamba na maafisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha pamoja kujadili imaandalizi ya ‘siku ya jumuia ya Afrika Mashariki’ katika maonesho ya ITB itakayo fanyika tarehe 6/2/2015.
men2Waionsehaji kutoka Tanzania wakiwa katika mazungumzo ya Kibiashara na wenzao kutoka nchi mbalimbali katika sikuu ya kwanza ya maonesho ya ITB jijini Berlin Ujerumani.
men3Waoneshaji kutoka taasisi za umma wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mweneshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi (wa tatu kulia) na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa Kwanza kulia) wakiwa katika kaunta ya banda la Tanzania katika maonesho ya ITB Ujerumani.
………………………………………………………………………….
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin
Maonesho ya Utalii ya kimataifa ya ITB ya siku tano yameanza leo jijini Berlin . Maonesho haya yanayofanyika kila mwaka na ambayo ni makubwa kuliko yote duniani yanahudhuriwa na waoneshajio zaidi ya 10000 kutoka nchi 190 duniani.
Tanzania katika maonesho haya inawakilishwa na waoneshaji 160 kutoka katika makampuni 60 kutoka sekta ya umma na binafsi . Taasisi za serikali zinazoshiriki maonesho haya ni Idara ya Utalii ya Wizara ya Maliaslili na Utalii, Bodi ya utalii Tanzania (TTB) ambao ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya. Nyingine ni Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya hifadhi ya ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Jumuia ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania idadi ya makampuni na taaisi yanayoshiriki kutoka Tanzania katika onesho la ITB imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo mwaka huu washiriki ni sitini (60) wakati mwaka jana jumla ya makampuni yalikuwa hamsini na tatu (53).
Miongoni mwa matukio muhimu yanayotarajiwa ni pamoja na tukio la siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki katika maonesho haya litakayofanyika tarehe 6/2/2015 ambapo Tanzania kama mwenyekiti wa jumuia hiyo itakuwa mwenyeji wa tukio hilo litafanyika katika banda la Tanzania. Mawaziri wa Utalii kutoka nchi wanachama, mabalozi wa nchi hizo hapa Ujerumani na wageni wengine mbalimbali waalikwa wanatarajiwa kujumuika na mwenyeji wao Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo katika banda la Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA